JAMII YAOMBWA KUMPA NAFASI YA UONGOZI MTOTO WA KIKE ILI ATIMIZE NDOTO ZAKE
Jane Sembuche
Na Mussa Augustine.
Mkurugenzi Mkazi wa Plan International Tanzania Jane Sembuche ameiomba jamii kumpa nafasi mtoto wa kike katika kuwania nafasi za uongozi ili kuweza kutimiza ndoto zake za masuala ya uongozi.
Sembuche ametoa rai hiyo leo Oktoba 10, 2024 Jijini Dar es salaam kwenye hitimisho la kampeni ya chukua hatamu( Girls takeover) inayotekelezwa na shirika hilo kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania ,ambapo limehudhuriwa na wasichana wapatao 40 kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania.
"Siku yetu ya leo ambayo tunaiita Girls takeover au wasichana kushika hatamu ni kampeni ambayo Plan International kwa Tanzania na Nchi mbalimbali Duniani ambapo Plan ipo hua tunafanya kila mwaka ikiwa ni sambamba na kusherehekea siku ya watoto wa kike duniani ambayo hufanyika Oktoba 10,kila Mwaka" amesema.
Aidha amesema kuwa wasichana wanaweza kuwa viongozi wazuri katika jamii,nakwamba kitu cha msingi ni kuweka juhudi ,malengo na kujiamini yeye kama msichana anaweza kufikia malengo yake na anaweza kua kiongozi katika jamii na kuleta mabadiliko yanayotakiwa.
Akizungumzia uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba mwaka huu Mkurugenzi huyo Mkazi wa Plan International Tanzania amesema kuwa pamoja na shirika hilo kutekeleza Kampeni ya Girls takeover lakini pia lina kampeni nyingine ya "Sikia Sauti zetu " ili kuwezesha sauti za wasichana sehemu mbalimbali wanahamasika kuzungumza nakuleta changamoto zao katika sehemu husika.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni