Zinazobamba

WAZIRI MCHENGERWA AZIAGIZA DART NA UDART KUSHIRIKISHA KAMPUNI ZA WAZAWA KUONDOA CHANGAMOTO YA UHABA WA MABASI YA MWENDOKASI

Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kadi Janja za Kukatia tiketi za Mabasi yaendayo haraka Jijini Dar es salam

Na Mussa Augustine.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)  Mh.Mohamed Mchengerwa ameagiza Wakala wa Mabasi yaendayo haraka (DART) kushirikiana na  Watoa huduma za Usafirishaji wa Abiria katika jiji la Dar es Salaam na Pwani (UDART) kuhakikisha  kampuni za Watanzania zenye uwezo wa Kuwekeza  katika Mradi wa mwendokasi zinapewa fursa hiyo ili kuweza kuondoa adha ya uhaba wa Mabasi.

Agizo hilo amelitoa leo Septemba 2,24 Jijini Dar es salaam wakati akizindua  mfumo wa kununulia tiketi kupitia kadi janja na mageti janja kwa ajili  ya Mabasi yaendayo haraka ambapo amebainisha kuwa  kwa sasa  kuna uhaba wa Mabasi yaendayo haraka yapatayo 670 nakwamba Hadi kufikia Mwezi Desema Mwaka huu yawe yameshanunuliwa.

Aidha amesema kwamba DART na UDART wanapaswa kuwashirikiasha wawekezaji wazawa ili kusaidia kuondoa changamoto hiyo ambayo inawakumba wananchi  wanaotumia usafiri huo.

"Lazima tukiri kwasasa tuna changamoto ya uhaba wa Mabasi, bado kuna miradi inaendelea ni vyema kuwaleta wawekezaji wazawa kuja kuwekeza kwani uwezo wanao ,watatusaidia kuondoa changamoto ya usafiri jijini Dar es Salaam, kuliko kukaa kuwasubiri wawekezaji kutoka nje ya nchi"amesema.

Nakuongeza kuwa "Wazabuni wa kitanzania wanauwezo Mkubwa  wa kutoa huduma za usafirishaji kwani kuna kampuni zinatoa huduma za Mabasi ya kwenda Mikoani zaidi ya 20, ambapo inahudumia Mikoa yote, hivyo ni vyema kuwaleta hawa wazawa kukabiliana na changamoto hii.

Aidha, Waziri Mchengerwa amefafanua kuwa kutumika kwa kadi janja kukata tiketi itarahisisha kupata huduma za usafiri kwa haraka zaidi pamoja na kutekelezaji  agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan la kuwahudumia Wananchi,pamoja na agizo la  Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania la kutaka kuanzishwa kwa Mfumo wa kukata tiketi kwa kutumia kadi janja.

"Kadi hizi zitasaidia kuokoa muda kwa abiria na kuondoa changamoto ya malalamiko ya watu kukaa muda mrefu kwenye Vituo kukata tiketi,lakini pia Mfumo huu utasaidia kutunza Mazingira ya Jiji la Dar es salaam" amesisitiza 

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Dart Athuman Kihamia amesema kadi hizo niza kisasa, zina ubora ambao ni tofauti na zile zinazotumika uwanja wa Taifa, nakwamba DART imeanza  kwa awamu ya kwanza lakini kadi hizo zitatumika  kwa awamu zote sita za Utekelezaji wa Miradi ya Mwendokasi Nchini.

Kihamia amesema kuwa kadi hizo niza kukusanyia nauli nakwamba kwasasa wataachana na mfumo wa kutumia Makaratasi kwani Mfumo huo wa kizamani unasababisha Uchafuzi wa  Mazingira, nakuondoa  malalamiko ya abiria kuhusu kudai chenji za shilingi 50 zilizokuwa zikisumbua.


Hakuna maoni