Zinazobamba

KITENGO CHA KUSAFISHA DAMU HOSPITALI YA RUFAA TEMEKE CHAZINDULIWA.

DC Sixtus Mapunda(alitabasamu)akiwa amekata utepe  kuashiria uzinduzi wa Kituo cha Kusafisha Damu Hospitali ya Rufaa ya Temeke

Na Mussa Augustine.

Serikali kupitia Wizara ya Afya imeendelea Kuwahimizi Wananchi kufanya Mazoezi na kupunguza hali ya ulaji wa vyakula usiofaa ili kuweza kuepukana na Magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwemo Sukari,Shinikizo la Damu pamoja na Afya ya Akiri ambayo yamekua yakiongezeka kila siku.

Rai hiyo imetolewa leo Agost 12,2024 Jijini Dar es Salaam  na Mkuu wa Wilaya ya TEMEKE , Sixtus Mapunda wakati akimwakilisha Waziri wa Afya Mh.Ummy Mwalimu kwenye Uzinduzi wa Kituo Cha Kusafishia Damu wagonjwa wa Figo, pamoja na kupokea vifaa mbalimbali ikiwemo gari la kubebea wagonjwa pamoja na Bus la kukubea watumishi ikiwa lengo ni kuboresha utoaji wa huduma hospitalini hapo.

DC Sixtus Mapunda( mwenye suti nyeusi) akikabidhi funguo za gari ya kubebea wagonjwa kwa Mganga Mkuu Mfawidhi  Dkt Joseph Kimaro

Aidha DC Mapunda  amesema kwamba tafiti na tathmini zinaonyesha kuwa magonjwa yasiyo ya  kuambukiza kama vile Shinikizo la Damu,Sukari,pamoja Afya ya Akili yamekua yakiongezeka kutokana na ulaji usio faa na kutokufanya Mazoezi hivyo niwakati sasa Wananchi washiriki kufanya Mazoezi na kuacha kula vyakula  vyenye Chumvi Nyingi na Sukari Nyingi,Pombe kupita kiasi pamoja na Matumizi ya Tumbaku.

"Serikali imeanza kutekeleza Afua mbalimbali ili kukabiliana na Magonjwa haya ikiwemo kufanya uratibu jumuishi wa wagonjwa kuanzia ngazi za zahati pamoja na kutoa Elimu kwa Wananchi kupitia wataalamu wa Afya ili kusaidia kukabiliana na Magonjwa haya ambayo yamekua tishio kubwa kwa sasa"amesema DC Mapunda

Awali akitoa taarifa za Utoaji huduma wa Hospitali ya Rufaa ya TEMEKE, Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali hiyo  Dkt Joseph Kimaro amesema kuwa Hospitali hiyo toka kuanzishwa kwake Mwaka 1970 imepata mafanikio Makubwa licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali zinazoikabili kama vile Ufinyu wa eneo la Hospitali hiyo kwa ajili ya kuongeza miundombinu ya utoaji wa huduma kwa Wananchi.

" Tumepata mafanikio makubwa sana kwa sasa tunalaza wagonjwa miambili hamsini(250)hadi mia tatu(300) kwa siku,huku wagonjwa wa nje (OP) ni zaidi ya elfu mbili, hivyo kituo hiki cha kusafishia Damu tunachozindua leo tumepata msaada kutoka kwa wenzetu wa Mamlaka ya Bandari Nchini ( TPA) ambapo wametoa kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni miambili kwa ajili ya ukarabati mkubwa wa Jengo la kuweka Mashine,pamoja na shilingi milioni Kumi kwa ajili ya ununuzi wa vifaa kama vile Viti mwendo(Wheelschair? pamoja na vifaa vya Kusafishia Damu" amesema Dkt Kimaro.

Nakuongeza kuwa "Tunaomba  Wadau wengine wajitokeze kutusaidia ili tuweze kuboresha huduma za Wananchi wetu na kumuunga Mkono  Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye kwa miaka mitatu ya uongozi wake amewekeza pakubwa kwenye Sekta ya Afya na Wananchi wanapata huduma salama.




  





Hakuna maoni