Maagizo hayo ameyatoa Julai 16,2024  Mkoani Pwani katika ziara yake ya kutembelea kiwanda hicho kwa lengo la kujionea ufanisi wake katika uzalishaji wa dawa hizo.

Amesema nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo Msumbiji ,Kenya,Botwsana,Iswatin zimekua zikitumia dawa hiyo inayozalishwa na TBPL chini ya shirika la Taifa la Maendeleo (NDC).

“ Halmashauri 184 zote nchini na ndugu zangu wa Wizara Afya mnunue  Viwadudu hivi  kwa ajili ya kuweza kupambana na Ugonjwa Malaria kwani ugonjwa huu bado ni tishio ,”Amesisitiza.

Aidha Jaffo amelitaka Shirika la Taifa la Maendeleo Nchini(NDC)kuhakikisha linashirikiana na halmashauri zote kwa kununua dawa hizo pamoja na kutoa elimu kwa wananchi ili wzitumie kwani hazina kemikali za sumu.

“NDC ongezeni kasi ya kutoa elimu na kutafuta masoko kwani lengo ni kuwasaidia Watanzania,tumieni mikutano ya ALAT muwaelimishe waje kuchukua dawa  dawa yenu,mesema.
Pia  amesisitiza NDC kutoacha malengo yake mama ya kuzalisha viuadudu vya viluilui Malaria na kuongeza uzalishaji wa dawa zingine.


Awali akitoa taarifa ya Maendeleo ya Kiwanda hicho kwa Waziri Jafo,Mkurugenzi Mtendaji wa NDC,Dkt  Nicolas Shombe,amesema Malengo Makubwa ya kiwanda cha Biotec products limited(TBPL)ni kupambana na Ugonjwa wa Maralia.

"Tunazalisha Lita milioni sita  kwa mwaka,na lengi letu ni kuhakikisha  tusadie  watanzania na nchi zingine kuondokana na ugonjwa tishio wa Malaria.