PURA kutafuta maeneo mazuri yanayovutia wawekezaji
Na Mwandishi wetu
MAMLAKA ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imesema imekuwa ikitekeleza kauli mbiu ya Tanzania Mahali sahihi pa Biashara na Uwekezaji kwa kujenga mazingira bora yanayovutia wawekezaji.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Makuu wa PURA, Mhandisi Charles Sangweni wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya 48 ya kimataifa ya Biashara sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya mwalimu Julias Nyerere Jijini Dar es salaam.
"Sisi kama Taasisi ya Serikali tumekuwa tukitekeleza kauli mbiu hiyo kwa kujenga mazingira bora yanayovutia wawekezaji ambao ndio makampuni yanayokuja kufanya tafiti katika eneo la mkongo wa juu wa Petroli"amesema Mhandisi Sangweni
Amesema katika kuendeleza shughuli za utafiti PURA inategemea
mpaka mwishoni mwa mwaka huu au mwaka 2025 inatarajia kutatagaza maeneo mbalimbali ambayo yataweza kuvutia wawekezaji kwa ajili ya kuja kushirikiana na PURA na kampuni Tanzu la Shirika la Maendeleo ya Patroli nchini (TPDC) kwenye kutafuta mafuta.
Amesema kuwa Tanzania ina viashiria vya kuwepo mafuta katika eneo la ukubwa wa skwea kilomita 534,000.
Aidha amesema hayo ni matokeo ya utafiti wa awali huku akisema eneo hilo ni asilimia zaidi ya asilimia 50 ya eneo lote la Tanzania lenye ukubwa wa skwea kilomita karibu 900,047.
"Hapa nchini tumefanya tafiti za awali katika maeneo mbalimbali ,ikumbukwe kwamba nchi yetu ukubwa wake inakava skwea kilomita karibu 900,047, kati ya hizo tafiti tulizofanya maeneo yenye viashiria vya kuwepp mafuta ni eneo la skwea kilomita 534,000.
Vilevile amesema kuwa kutokana na mabadiliko ya tabianchi ambayo yamefanya Dunia yote inataka kibafilisha mwelekeo kutoka kwenye matumkzi ya nishati chafu na kwenda kwenye matumizi ya nishati safi ,Tanzania nayo ipo kwenye muelekeo huo.
"Tunafahamu kwamba dunia inabadilika,kwenye upande wa nishati dunia yote inaongelea nishati safi na inataka kutoka kwenye nishati hiyo ya petroli kwenda kutumia nishati ya hewa ambayo inazuia uchafuzi wa mazingira ,malengo ni kufika 2060 dunia iwe imefikia kwenye matumizi ya nishati jadidifu kwa kiasi kikubwa."
Amesema,kwa upande wa Tanzania malengo ya kufikia nishati safi ya kupikia kwa hadi asilimia 80 ifikapo 2034 huku akisema kuhama kwenye nishati ambayo inachafua hali ya hewa na kutumia nishati ambayo uchafuzi wake siyo wa kiasi kikubwa au haichafui kabisa.
"Sasa sisi kama watafutaji wa petroli ,ni wadau wakubwa kwenye hilo na katika hili sisi tunafanya tafiti mbalimbali za kuwezesha hili liwezekane,lakini wakati huo tunatafuta kiasi cha gesi ambacho ndiyo tuliyogundua hivi sasa hapa nchini."amesema Mhandisi huyo
Amesema gesi hiyo itasaidia kutumika majumbani ,kwenye magari na maeneo mengine ya uendeshaji mitambo kwa sababu gesi asilia iliyopo ambayo kwa sasa imegunduliwa Songosongo na Mnazibay imepitishwa duniani kama chanzo cha nishati ambacho kitatumika kwa kipindi cha mpito kuelekea matumizi ya nishati jadidifu.

No comments
Post a Comment