Zinazobamba

GRAND GALA DANCE KUFANYIKA AGOST 30 ,MGENI RASMI WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA.

Na Mussa Augustine

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Tamasha la Tatu la Grand Gala Dance litakalofanyika tarehe 30 mwezi wa nane katika Ukumbi wa Superdome Masaki Jijini Dar es salaam.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo tarehe 24, 2024  Mkurugenzi wa Kampuni ya Chocolate Princes Ltd ambayo imeandaa tamasha hilo, Mboni Masimba amesema kuwa Tamasha hilo ni kumuenzi baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere.

Amesema kuwa Tamasha hilo litahusisha wasanii wakubwa kutoka bendi nne za muziki wa Dansi ikiwemo  African Stars (Twanga pepeta) Fm Academia wazee wa Ngwasuma,Tukiyu Bendi pamoja na Malaika Bendi, chini ya Christian Bella, hivyo wapenzi mashabiki wa muziki wajitokeze kwa wingi katika Tamasha hilo.

"Tulipanga kufanya mwezi wa kumi kwa ajili ya Kumuenzi baba wa Taifa Hayati Mwalimu  Julius Nyerere,lakini tumebadilisha tutafanya mwezi wa nane tarehe 30, hivyo kwa sasa wananchi waendelee kununua tiketi ili wajumuike kwa pamoja siku hiyo" amesema Mboni.

Akizungumza Patcho Mwamba amesema kuwa kutakua na Burudani kubwa itakayotolewa na wasaniii hao nakwamba Tamasha hilo sio la kukosa.

" Tutawasha moto,muziki mkali na wananchi waje waone bendi inaimba mubashala( live) ni itakua ni siku nzuri sana waje washuhudie" amesesitiza Patcho Mwamba


Nae Charles Baba amesema siku ya Grad Gala Dance atafanya makubwa kwa kutoa Burudani ya kifani,hivyo mashabiki na wapenzi wa Burudani wajitokeze katika kuona Burudani hiyo.


No comments