Mtaalam Veta ashauri masomo ya ujuzi yapewe kipaumbele
Na Mwandishi wetu
Meneja mahusiano wa mamlaka ya elimu na mafunzo ya Ufundi stadi (VETA),
Mh. Sitta Petter amewashauri wazazi/walezi na wanafunzi wa kidato cha nne kwa
ujumla wake kuanza kufikilia kusoma mafunzo ya ufundi ili kujipatia ujuzi
wakati huu ambao wanasubiri matokeo ya kidato cha tano kutoka
Sitta ametoa rai hiyo Novemba 3, 2023 wakati akizungumza na
mtandao wa fullhabariblog katika uwanja wa mnazi mmoja ambako kulifanyika maonesho
ya miaka 50 ya Necta.
“Tuna vijana wengi ambao wamemaliza kidato cha nne ambao
wanasubiri matokeo kutoka, tunaamini wapo ambao watakwenda kidato cha tano
lakini pia wapo watakaokwenda vyuo vya ufundi, tunawaambia wakati huu ambao
wapo kipindi cha mpito watumie fursa hii kusoma kozi fupi za ufundi stadi,”
alisema
Amesema badala ya kuwapeleka watoto kusoma masomo kwa ajili ya
kidato cha tano (Pre-form five), basi watumie muda huo kujifunza ujuzi, kwani
mitaala ya sasa inasukuma Zaidi ufundi
Amesema faida ya kusoma ufundi stadi ni pamoja na kuwa katika
nafasi nzuri ya kupata ujuzi ambao utakusaidia katika Maisha yako, kwamba kijana
ambaye anao ujuzi anakuwa tofauti na yule ambaye bado hana ujuzi.
Mimi niko form five lakini tayari fundi umeme, au fundi magari,
inawezekana kabisa hata wakati wa likizo akirudi anaweza kuendeleza fani yake,
jambo hili linawezekana kabisa,” alifafanua
Mtoto anapokwenda kusoma Pre-form five halafu hakubahatika kufaulu
maana yake mzazi amekula hasara, lakini mtoto naye amepoteza muda wake, lakini
akipata ujuzi atakuwa msaada katika familia,” aliongeza
Mtaalam huyo wa masuala ya mahusiano ya umma amesisitiza kusema elimu
ya sasa ina mikondo miwili, upo ule wa kawaida lakini pia upo wa mafunzo ya
amali, ni vizuri wazazi wakalifahamu hilo na kuandaa Watoto watakaoingia katika
makundi hayo
Hakuna maoni
Chapisha Maoni