PSPTB yawataka Maafisa Ununuzi na Ugavi Kujisajili Kwenye Mfumo Mpya
|
|||
Hayo ameyasema leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari ambapo amebainisha kuwa ili kudhibiti ununuzi na ugavi usio na ubora, serikali imeamua kuanzisha mfumo mpya ambao kila afisa ununuzi na ugavi anapaswa kujisajili ili aweze kutambulika haraka anapobainika kukiuka taratibu za ununuzi.
Aidha Mbanyi amesema kwamba mfumo huo mpya unaoandaliwa na serikali nakusimamiwa na bodi hiyo utaruhusu maafisa ununuzi na ugavi waliosomea taaluma hiyo na kusajiliwa na PSPTB ndio pekee watakoingia kwenye mfumo huo wa manunuzi nakuwezesha kuwachukulia hatua wale wanaoshindwa kufuata taratibu za taaluma hiyo.
“ Tunamatumaini makubwa kuwa huu mfumo utasaidia kuondoa malalamiko yakuwepo kwa ununuzi usiofuata taratibu za sheria za ununuzi na ugavi nakupelekea serikali na skta binafsi kupata hasara,hivyo bodi inawataka maafisa ununuzi wote kuhakikisha wanajisajili katika mfumo huo haraka iwezekanavyo ili kuepukana na usumbufu unaoweza kujitokeza” amesema Mbanyi.
Hali kadhalika Mkurugenzi Mtendaji huyo w PSPTB amesisitiza kuwa hivi karibuni wataanza oparesheni maalumu yakukagua mashirika ya umma na binafsi kama yamesajiri wataalamu waliosomea taaluma ya ununuzi na ugavi pamoja na kusajiliwa na bodi hiyo.
Hata hivyo amefafanua kuwa ukaguzi huo utaanza kwa mashirika na taasisi kubwa za serikali na binafsi ikiwa lengo ni kuhakikisha wanawabaini wale wataalamu wa ununuzi na ugavi wasio na sifa na pia kuona kama hawajasajiliwa na bodi ili kuwachukulia hatua za kisheria.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni