Global Education Link Yawashauri Wanaotaka Kusoma Vyuo Vya Ulaya Kuchangamkia Fursa.
Na Mussa Augustine.
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link Abdumalik Mollel amewashauri wanafunzi wanaotaka kujiunga na Vyuo Vikuu vya nje ya nchi wachangamkie fursa katika nchi za Umoja wa Ulaya kama vile Georgia na Cyprus kwani nchi hizo zina fursa ya kupata ajira.Hayo ameyasema wakati akizungumza na Waandishi wa habari kwenye Ufunguzi wa Maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu,Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania(TCU) yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Mollel amesema kwamba nchi ya Georgia ina idadi ya watu takribani milioni nne,na kwamba inakumbwa na changamoto ya nguvu kazi kutokana nakuwa na idadi kubwa ya wazee ukilinganisha na idadi ya vijana,hivyo wanafunzi kutoka mataifa mengine ambao wanaenda kusoma kwenye nchi hiyo wanaweza kupata ajira kirahisi baada ya kuhitimu masomo yao.
"Georgia idadi ya watu takribani milioni nne,pia ni miongoni mwa nchi tajiri duniani,nje tu ya kusoma kwenye nchi hiyo pia unapata ajira,kuna changamoto ya nguvu kazi kwani wengi ni wazee,ili nchi yao iendelee kupiga hatua wanahitaji nguvu kazi ,ili watoto wetu wanaosoma pale wanaweza kuwatosheleza kwa ajira" amesema Mollel.
Aidha amendelea kufafanua kuwa wanafunzi wanaosoma kwenye nchi hizo za Ulaya wanaweza kupata Visa ya Shengen ambayo inawapa fursa ya kuzunguka nchi zipatazo 30 ikiwemo Italia, Ujerumani, Ufaransa, Hungary na Poland ambapo nchi hizo ni kubwa zenye teknolojia kubwa lakini pia zina changamoto ya idadi ya watu hivyo zinahitaji nguvu kazi.
" Kwa wakati mwingine Global Education Link tumeona tuvilete Vyuo Vikuu vya Ulaya hapa kwenye maonesho ili kuwasaidia vijana kuomba kwenda kusoma kwenye nchi hizo, lengo letu siyo wanafunzi wanaenda kusoma nje ya nchi warudi na chetu tu bali tunataka warudi na wawekezaji,tunataka warudi na fursa ya Uwekezaji nakutusaidia kuajiri vijana wenzao na kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira" Amesema Mollel.
Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa changamoto zinazowakumba vijana wakitanzania kukosa ufadhili wa nafasi za masomo nje ya nchi ni pamoja na kuchelewa kutuma maombi British Council hivyo kupelekea fursa waombaji wachache kupata fursa hiyo,ambapo amewasisitiza watume maombi mapema.
Hata hivyo ameongeza kwamba nchi ya India ina vyuo vya Elimu ya juu vipatavyo 80,000 na kwamba ndani ya nchi hiyo kuna Vyuo vyenye kampasi zaidi ya Moja vyenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 40,000 vikijitofautisha na Vyuo vingine duniani
Meneja wa Kitengo Cha Mitihani kutoka British Council-Tanzania, Henry Sangilwa. |
Kwa upande wake, Meneja wa Kitengo Cha Mitihani kutoka British Council-Tanzania, Henry Sangilwa amesema kuwa lengo la kuja kwenye maonesho hayo ni kuwaletea habari njema za fursa za ufadhili wa masomo zinazopatikana Nchini Uingereza.
Pia amefafanua kuwa kila mwaka nafasi za ufadhili zipatazo 35 za wanafunzi kwenda kusoma nchini humo hutangazwa lakini idadi ya watanzania wanaojitokeza kuomba kwenda kusoma ni ndogo,hivyo amewasisitiza kuchangamkia fursa hiyo ambapo dirisha la udahili litafunguliwa kuanzia mwezi Agosti hadi Novemba.
" Vigezo vinapimwa kuanzia kuzungumza lugha ya Kiingereza ambapo hufanywa na British Council " amesema Sangilwa.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni