WANA GDSS WAFANYA UCHAMBUZI NA KUANGALIA USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI KATIKA UUNDAJI WA BAJETI YA TAIFA
Washiriki wa semina za jinsia na maendeleo (GDSS) wamekutana jumaatano hii lengo likiwa ni kujadili ushirikishwaji wa moja kwa moja wa wananchi katika upangaji wa bajeti kuu ya taifa.
Mlaghbishi wa semina ya GDSS wiki hii Bw. Hancy Orote akitoa ufafanuzi juu ya jambo fulani katika semina iliyofanyika mapema wiki hii makao makuu ya TGNP Mtandao Mabibo Dar es salaam. |
Akiongoza semina hiyo mwanaharakati kutoka GDSS Bw. Ance Obote alisema dhumuni la kukutana mahali hapo ni wanaharakati kubadilishana uwezo kuhusu ufahamu, ushiriki na jinsi gani wanatoa elimu hiyo kwa wananchi kuhakikisha wanaitumia haki yao ya msingi ya kushiriki katika bajeti.
Muwezeshaji huyo amesema kuwa wananchi huusika sehemu kuu mbili ambazo ni kwenye kupanga vipaumbele na ufuatiliaji(utekelezaji) lakini wananchi hawapewi nafasi ya kupanga vipaumbele na kinachofanyika ni diwani anakutana na mtendaji wa kata na kupanga kipi kianze kama kipaumbele na kipi kiwe cha mwisho.
Mshiriki wa semina za GDSS Bw. Geofrey Chambua akitoa mchango wake katika semina iliyofanyika mapema wiki hii Mabibo jijini Dar es salaam. |
Na jambo lingine ni kwamba kwa maeneo ya mijini hakunaga vikao vinavyokaliwa na kujadili maendeleo ya mtaa ama kata hivyo mambo yanaendeshwa kienyeji na mambo mengi yanayofanywa yanakuwa ni akili za viongozi na siyo mawazo ya wananchi hali inayoweka ugumu katika utekelezaji wa mambo mengi kama hili la kuweka vipaumbele.
Aidha wanaharakati wameamua kuweka utaratibu wa kujipima kwa kuangalia harakati zao zinafika umbali gani na katika hili wameamua kupeleka ushawishi katika kata walau tatu na kuja kuangalia ushawishi wao wa kubadilisha dhana hii ya viongozi kupanga vipaumbele wenyewe bila kushirikisha wananchi inaweza kuisha?.
Bw. Msafiri Shabani akitoa maoni yake ya nini kifanyike ili kuhakikisha wananchi wanapata haki yao ya moja kwa moja ya kushiriki katika kupanga vipaumbele katika bajeti ya Taifa. |
Lakini pia kupitia semina hiyo wanaharakati wameweka mipango mbalimbali ya kufuatilia jambo hilo na kugawana majukumu mpaka ifikapo tarehe 29 novemba kila kundi lililochaguliwa kufuatilia katika kata husika liwe limeleta mrejesho wa kilichopatikana na mgawanyo wenyewe ulikuwa kama ifuatavyo.
Washiriki wa semina za GDSS wamepewa majukumu ya kufuatilia katika serikali zao za mitaa kwa kuwahoji viongozi wa mitaa yao na kuleta mrejesho kwanini wananchi hawapati nafasi ya kushiriki katika kupanga vipaumbele na matokeo yake wanahusishwa katika hatua za mwisho ambazo ni utekelezaji.
Baadhi ya washiriki wa semina za GDSS walioudhulia mapema wiki hii. |
Lakini vituo vya taarifa na maarifa wao wameombwa kufuatilia serikali kuu hii ikiwa ni katika wizara mbalimbali zinazohusika na hili ili kuweza kukusanya majibu ya serikali za mitaa pamoja na wizara kuweza kuwa na jibu moja lililokamilika kuhusu swala hilo.
Na jambo lingine ni kuabadilisha mtindo wa kuingia katika sekta hizi kwani wengi uenda kwa njia ya kujiita wanaharakati jambo ambalo linawafanya watu hawa kuwaona wao ni wapinzani na kuweka chuki miaongoni mwao, na pia imeelezwa sio vizuri kwenda mtu mmoja mmoja na wanatakiwa kuunda makundi madogo madogo yatakayowafanya waonekane ni wananchi kweli wanaohitaji taarifa za kata au mtaa wao.
Baadhi ya wanaharakati wakifuatilia kwa umakini semina iliyoendeshwa na Hancy Orote mapema wiki hii Mabibo Dar es salaam. |
Aidha wanaharakati wameshauriwa kufanya kazi kwa moyo wa kijitolea na kuleta mabadiliko katika jamii yao na siyo kufanya ili waonekane na TGNP au kwa ajiri ya kuleta ripoti kwa mtu Fulani bali wafanye kwa manufaa yao na jamii iliyowazunguka.