Home
/
Unlabelled
/
ASKOFU SHOO AWA NI KIONGOZI WA KWANZA WA KIROHO KUZUNGUMZIA TUKIO LA KUPIGWA RISASI TUNDU LISSU,SOMA HAPO KUJUA
ASKOFU SHOO AWA NI KIONGOZI WA KWANZA WA KIROHO KUZUNGUMZIA TUKIO LA KUPIGWA RISASI TUNDU LISSU,SOMA HAPO KUJUA
Aliyekua Askofu wa Kanisa la TAG Mkoa wa Kilimanjaro, Gloroius Shoo amesema kitendo cha kupigwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kumeitia doa nchi.
Alisema nchi itapoteza sifa ambayo iliijivunia ya kuitwa kisima
cha amani kwa miaka mingi duniani kutokana na vitendo viovu
vinavyozidi kujitokeza vya umwagikaji wa damu pamoja na utekaji unaoendelea kwa sasa.
Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake leo Jumamosi Askofu Shoo amesema sifa ya amani imesababisha watu mashuhuri kuja nchini pamoja na ujio wa wawekezaji wengi bila kuhofia usalama wao kutokana na amani iliyokuwepo.
Shoo amesema kuwa watu waliofanya unyama huo walikua na kiburi kikubwa kutokana na uthubutu wao wa kufanya mchana katikati ya makao makuu ya nchi.
“Ninakemea vikali umwagikaji wa damu kwa viongozi wetu, huu ni udhalilishaji mkubwa na haukubaliki kwa taifa hili la
Tanzania, ninaomba Serikali kwa nguvu zote ihakikishe inawatia mikononi wote wanaohatarisha usalama wa nchi yetu,” alisema Askofu Shoo.
“Uthubutu huo lazima uingiliwe kati na Serikali la
sivyo itatuondolea sifa ya nchi yetu na huu ni udhalilishaji
mkubwa.”
ASKOFU SHOO AWA NI KIONGOZI WA KWANZA WA KIROHO KUZUNGUMZIA TUKIO LA KUPIGWA RISASI TUNDU LISSU,SOMA HAPO KUJUA
Reviewed by Unknown
on
18:19:00
Rating: 5