RAIS CHUO CHA USAFIRISHAJI AMPONGEZA MAGUFURI
Rais wa serikali ya wanafunzi chuo cha Taifa cha usafirishaji (SONIT) Bw. Stambuli Mombeki Kaiza (PICHA MAKTABA) |
Rais
wa serikali ya wanafunzi wa chuo cha Taifa cha usafirishaji (NIT) Stambuli
Mombeki amesifu uzinduzi
wa mradi wa ujenzi, ukarabati na upanuzi
wa bandari ya Dar es Salaam uliofanywa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania akisema kuwa mradi huo utasaidia watanzania wengi kuinuka kimaendeleo
ikiwamo wahitimu wa sekta ya usafirishaji kupata ajira
“Serikali ya wanafunzi ya chuo cha
Taifa cha usafirishaji SONIT tunapongeza jitihada za Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania John Magufuli kwa jitihada zake anazofanya, lakini Zaidi ni
kuhusu upanuzi wa bandari ya Dare salaam kwani tunaamini ajira nyngi za moja
kwa moja na ambazo si za moja kwa moja zitapatikana” Alisema Mombeki
Akizungumza na Mtandao wa FULLHABARI
BLOG Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa chuo hicho Bw. Stambuli Mombeki amesema wao
kama wanafunzi wa sekta ya usafirishaji wameguswa na jitihada zinazofanywa na
Rais katika kuimarisha miundombinu ya usafirishaji Nchini na kwamba wao kama
nguvu kazi iliyobobea katika utaalamu wa usafirishaji wanaamini wana kila
sababu ya kupaza sauti zao za kuunga mkono jitihada hizo.
Hivi karibuni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania John Maguli aliweka jiwe la msingi la uzinduzi wa ujenzi, ukarabati na upanuzi wa bandari ya
Daresalaam.
Hafla hiyo ilfanyika mwanzoni mwa
mwezi wa huu katika eneo la bandari Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na
viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof.
Makame Mbarawa Mnyaa, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage,
Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke na Mwakilishi wa Benki ya Dunia Bi.
Bella Bird.
Rais
Magufuli alibainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuboresha
bandari zote nchini lakini ameitaka TPA na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
kuongeza udhibiti wa mizigo inayoingia na kutoka kupitia bandari kwa
kuhakikisha mizigo hiyo inakuwa halali na inalipiwa kodi ipasavyo.
Ujenzi,
ukarabati na upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam umepangwa kufanyika kwa miezi
30 kuanzia sasa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 926.2 ambapo kati yake,
Shilingi Bilioni 132 zinatolewa na Serikali ya Tanzania, Shilingi Bilioni 770
ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia na Shilingi Bilioni 24 ni
Msaada kutoka Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID).
Kazi
za ujenzi, upanuzi na ukarabati huo zitafanyika katika gati namba 1 hadi gati
namba 7 ambazo zinaendeshwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)
na zitahusisha kujenga gati hizo, kuongeza kina cha bahari kwa kuongeza urefu
kutoka wastani wa mita 12 hadi kufikia mita 15.5 na kukarabati miundombinu
wezeshi ya bandari.
Mradi
huu mkubwa utaiwezesha bandari ya Dar es Salaam kuongeza uwezo wa kuhudumia
meli kubwa kutoka meli zenye urefu wa meta 243 na uwezo wa kubeba makontena
kati ya 2,500 na 4,000 hadi kufikia meli zenye urefu wa meta 320 na uwezo wa
kubeba makontena kati ya 6,000 na 8,000 na pia kuongeza uwezo wa kuhudumia
shehena za mizigo kutoka tani Milioni 18 za sasa hadi kufikia tani Milioni 28
ifikapo mwaka 2022.
Akizungumza
kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi huo, Rais Magufuli amewashukuru wadau
wa maendeleo walioshiriki kufanikisha mradi huo ambao ni Benki ya Dunia na DFID
na amesema mradi huu ukikamilika utaiwezesha bandari kuwa ya mfano, na ametaka
wakandarasi wanaojenga mradi huo waukamilishe haraka ikiwezekana kabla ya miezi
30 kuisha ili Tanzania na nchi za Rwanda, Uganda, Burundi, Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Zambia, Malawi na Zimbabwe zianze kunufaika
mapema.