MASIKINI MALINZI NA WENZAKE,KESI YAO YAPIGWA KALENDA TENA,SOMA HAPO KUJUA
Kesi inayomkabili Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, TFF, Jamali Malinzi na wenzake imeendelea leo July 31, 2017 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusogezwa tena mbele hadi August 11, 2017 kwa sababu upelelezi haujakamilika.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi haujakamilika ambapo hata hivyo, Mawakili wa washtakiwa, James Bwana na Abraham Senguji hawakuwa na pingamizi na suala la upelelezi.
Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi August 11, 2017.