Maonyesho ya vyuo vikuu yafunguliwa Dar...CHUO CHA ACHARYA CHATANGAZA FURSA ZILIZOPO...YAWAKARIBISHA WATANZANIA KUTEMBELEA BANDA LAO
Ganesh G akifafanua jambo kwa Mwandishi wa habari mapema hivi karibuni... Meneja huyo amewakaribisha watu kwenda kupata taarifa muhimu kuhusiana na chuo cha Acharya kilichpo Nchini India |
Mwandishi wetu
Meneja uhusiano wa Taasisi ya Acharya Institute of Technology hapa Nchini Bw.Ganesh G amesifu maandalizi ya ufunguzi wa maonesho ya 12 ya vyuo vikuu vya ndani na Nje ya Nchi na kuwataka watanzania hususani wazazi kuwa kutumia fursa hiyo kuchagua vyuo vyenye ubora unaokubalika ili ndoto za watoto wao ziweze kutimizwa.
Akizungumza na Mtandao wa Fullhabari blog..Ganesh G amesema suala la kutafuta chuo chenye ubora ni lazima...kwani makosa yatakayofanywa sasa yataweza kugharimu maisha ya mtoto katika kipindi cahke chote cha maisha.
AFAFANUA UBORA WA ACHARYA INSTITUTE OF TECHNOLOGY
Akizungumzia kuhusu uobora wa chuo cha Acharya, Ganesh G amesema chuo hicho ni chuo pekee ambacho kinatoa elimu bora yenye gharama ndogo ukilinganisha na vyuo vingine duniani, na kwamba hata utaratibu wake wa kujiunga ni mwepesi.
Amesema Acharya ni sehemu salama ya kuwekeza kielimu kwa mtoto wako, kwani mtoto anafundishwa vitu kimatendo na kwamba akimaliza masomo katika chuo hicho mtoto anakuwa yuko vizuri si tu Darasani lakini pia kivitendo.
"Sisi tunafundisha kwa mfumo wa vitendo zaidi...miezi mitatu darasani mwezi mmoja mwanafunzi anafanya kazi ya kile alichosoma katika makampuni mbalimbali kule India...tunahakikisha mwanafunzi alichosoma ndicho anachokielewa na kwa kufanya hivyo wanafunzi wetu wamekuwa na ufanisi wa hali ya juu katika kazi...na niseme wazi kwa kweli wanafunzi wetu wamekuwa ni mabalozi wazuri sehemu za kazi" alisema Ganesh G
Akizungumzia Idadi ya watanzania ambao mpaka sasa wameweza kusoma katika chuo hicho ni kufanikiwa, Ganesh G amesema tayari zaidi ya wanafunzi 500 wamepita katika chuo hicho mmoja wapo akiwa ni aliyewahi kuwa msemaji wa chama cha mapinduzi na Waziri wa habari, utamaduni na michezo Bw. Moses Nape Nnauye.
AOMBA WATU KUTEMBELEA BANDA LAO
Aidha katika hatua nyingi, Ganeshi G amewakaribisha wakazi wa jiji la Daresalaam kutembelea banda lao lililopo katika maonyesho hayo ili kupata taarifa nzuri kuhusiana na chuo hicho.
Ganesh amesema kupanga ni kuchagua...watu wanapaswa kuchagua kilicho bora na kwamba Acharya ni suluhisho la kilicho bora
Maonyesho hayo yamefunguliwa na WAZIRI Mkuu, Kasimu Majaliwa huku akiwataka vyuo vyote vya umma kutoza shilingi 10000 kama ada ya kuombea udahili.
Katika maonyesho hayo ya 12, Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU), imevitaka baadhi ya vyuo hapa nchini kusimamisha baadhi ya masomo.