MAAMUZI YA MAHAKAMA KUHUSU KESI ZA WABUNGE 8 WALIOFUKUZWA UANACHAMA,SOMA HAPO KUJUA
Leo July 28, 2017 Mahakama Kuu ya Tanzania imepanga kusikiliza kesi ya Wabunge 8 wa Chama cha Wananchi CUF ambao wamevuliwa Uanachama na Mwenyekiti wa Chama hicho Prof. Ibrahim Lipumba kuwa ni August 2, 2017.
Kwa mujibu wa Wakili wa Wabunge hao, Peter Kibataka kesi hiyo imepangwa kusikilizwa mbele ya Jaji Lugano Mwandambo.
Katika kesi hiyo maombi yatakayosikilizwa ni zuio la Utekelezaji wa mchakato wa kuwaapisha Wabunge wanane Wateule wa Viti Maalum wa CUF pamoja na kuzuia utekelezaji wa Maamuzi ya Baraza Kuu la CUF.