KIFO CHA WAZIRI WA ULINZI WA KENYA ,CHAMTOA MACHOZI LOWASSA,SOMA HAPO KUJUA
Waziri Mkuu
wa zamani, Edward Lowassa ametuma salamu la rambirambi kufuatia kifo cha Waziri
wa usalama wa Kenya, Meja mstaafu Joseph Nkaissery aliyefariki ghafla katika
hospitali ya Karen iliyopo Nairobi muda mfupi baada ya kupelekwa kwa uchunguzi.
Meja Joseph
Nkaissery alipelekwa hospitali kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kiafya kabla
ya umauti kumkuta, Mkuu wa Utumishi wa Umma wa Kenya Joseph Kinyua
amethibitisha kutokea kwa kifo cha Waziri wa Ulinzi wa Kenya.
Baada ya
taarifa hizo kusambaa Waziri Mstaafu Edward Lowassa amesema Nkaissery alikuwa
ni rafiki mzuri na kiongozi mzuri na wakupigiwa mfano
"Natuma
salamu zangu za pole kwa familia na watu wa Kenya kwa kumpoteza Waziri Joseph
Nkaissery, alikuwa ni rafiki mzuri na kiongozi mzuri wa kupigiwa mfano, Mungu
amumlaze mahali pema peponi" alisema Lowassa
Joseph
Kasaine Ole Nkaissery alikuwa ni mwanasiasa wa Kenya, Mbunge kutoka mwaka 2002
mpaka 2014 na baadaye aliteuliwa kuwa Waziri wa usalama wa Kenya mpaka kifo
chake, mbali na hilo Nkaissery alikuwa kiongozi Mkuu wa jamii ya Maasai nchini
Kenya.
Advertisement