HALIMA MDEE AJIRIBUA TENA,ASEMA MAMBANO YA KUDAI HAKI YANAENDELEA,SOMA HAPO KUJUA
Mbunge wa Kaw, Halima Mdee baada ya kuachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni 10 kwa kudaiwa kutoa lugha chafu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewashukuru wote waliopaza sauti zao ili haki itendeke kwake huku akisema mapambano bado yanaendelea.
Halima mdee ametumia ukurasa wake wa Tweeter kutweet shukrani hizo huku akisema mapambano yanaendelea.
Mhe. Halima ametweet
Kwa heshima KUBWA niwashukuru sana wote mliopaza sauti zenu kutaka haki itendeke kwangu na kwa watoto wetu wa kike! #Mapambano yanaendelea!
Halima Mdee alidaiwa kutoa maneno hayo ya kukashifu na ya uchochezi katika mkutano wake wa Baraza la Wanawake Chadema uliofanyika katika ofisi za baraza hilo wakati akizungumza na wanahabari.