Zinazobamba

TECNO MOBILE YAWAKUTANISHA VIJANA NA JOKATE,SOMA HAPO KUJUA

Kampuni ya simu ya TECNO Mobile iliandaa futari kwaajili ya vijana wenye kupitia changamoto za kimaisha kutoka kwenye kituo cha “Watoto wetu, Donbosco” pamoja na wadau wake. 
 Hafla hiyo ilifanyika maalumu kwaajili vijana walio katika mazingira magumu pamoja na balozi wa simu hiyo. Waalikwa waliungana pamoja na mrembo,mjasiriamali na mwanamitindo Jokate Mwegelo katika Futari maalumu hiyo  iliyo sheheni michezo,zawadi kemkem.

Pia Zawadi za simu ya Camon Cx zilitolewa kwa washindi wa kampeni ya #SelfieKamili, kampeni ya Tecno Camon cx ni kampeni inayoendeshwa na Kampuni hiyo kupitia simu yake mpya ya camon Cx inayosifika kwa kua  na kamera kubwa ya 16 megapixel

Tecno Mobile iliandaa futari hii maalumu ili kuwapa nafasi  vijana walio katika mazingira  magumu kujumuika na balozi wao wa simu hiyo pamoja na washindi wa  simu ili kubadlishana mawazo huku wakipata futari mahsusi ilyoandaliwa kwaajili yao. 


Tecno inawasaa wateja wake kuendelea kufatilia mitanndao yao ya kijamii ili kundelea kupata zawadi hasa kipindi kijacho cha sikukuu ya eid, zawadi hizi zipo kwa kila atakaeshiriki na kuzingatiwa vigezo.