Zinazobamba

MSTAHIKI MEYA AFICHUA KILICHOMSUKUMA KUFUTURISHA DAR



MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ametaja sababu ya kuendelea na utaratbu wake wa kufuturisha wakazi wa Jiji hilo kuwa ni kuonyesha upendo alionao kwao na pia kufanya ofisi yake iwe kimbilio la wananchi wote bila kujali dini zao, makabila yao na itikadi ya vyama vyao.
Akizungumza na mtandao wa Fullhabari, Meya Isaya Mwita amesema dhamira yake kubwa ni kuona kuwa anaweza kushirikiana vema na wakazi wa Jiji la Daresalaam na kwamba hiyo inaenda sambamba na kuheshimu mila, desturi na utamaduni wa Wanadaresalama.
“Nimekuja Mji huu tumekuta watu wanautaratibu wao, ninakila sababu ya kuheshimu mila zao, utamaduni wao ambao nimeukuta kwani kufanya hivyo kunaongeza upendo kati yetu” Aliongeza.
Aidha Mwita amesema mafanikio ya kufuturisha wakazi wa Daresalaam kwa miaka miwili mfululizo ni ishara tosha kuwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam ni watu wanaopenda umoja na ni wako tayari kushiriki katika jambo lolote lenye heri.
Alisema Wakati anajipanga kuandaa futari kwa wakazi wa Jiji alikuwa na wasiwasi kama kweli watu wangeweza kuhudhuria, lakini akajipa matumaini kwamba watu wa Daresalaam ni wakalimu na bila shaka wangeweza kufika katika hafla hiyo
Na ukweli watu wamefika kwa wingi jambo ambalo amesema anamshukuru mungu kwa kuwezesha futari hiyo kufanikiwa. “Kwa kweli kipekee kabisa naomba nimshukuru kadhi Mkuu wa Tanzania bara Abddallah Yusuph Mnyasi kwa kutenga muda wake na kuja kushiriki nasi hapa…ni jambo zuri licha ya umri wake kumtupa mkono lakini amesema lazima afike katika hafla hii, ni heshima kubwa amenipa” aliongeza .
Mstahiki Meya wa Jiji la Dare salaam Isaya Mwita Ijumaa aliwafuturisha wakazi wa jiji la Dar es Salaam zaidi ya 600
kutoka sehemu mbalimbali jijini hapa nakutumia nafasi hiyo kuwatakia waumini wote wa dini ya kiisilamu heri ya kumalizia Ibada ya funga ya Mwezi Mtukufu wa Radhani sambamba na kuingia kwenye sikukuu ya Idi.
Aidha Mashehe wa jiji la Dar es Salaam waliohudhuria Futari hiyo jana walimpongeza Meya Mwita kwa kuandaa Futari hiyo na kusema kuwa ni jambo la heri kwao na hivyo wataendelea kumuunga mkono katika shuguli zake za kuwaongoza wananchi kwa ajili ya kuwaletea Maendeleo.
Hafla hiyo ambayo ilihudhuriwa na Kadhi Mkuu wa mkoa , Mashehe wa jiji la Dar es Salaam, viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa, makundi mbalimbali ya kijamii, ilifanyika katika viwanja vya Karimjee jijini hapa.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa Futari hiyo jana Meya Mwita alisema kuwa kupitia mfungo wa Ramadhani wakazi wa jiji na watanzania wote kwa ujumla wanapaswa kuzidisha hali ya unyenyekevu, uchamungu ili kutenda mambo yaliyomema na hivyo kusherehekea sikukuu ya Iddi kwa hali ya utulivu.
Meya Mwita alifafanua kuwa kupitia hafla hiyo imekuwa ni fursa ya kipekee kujumuika pamoja na wananchi wa jijini hapa kuzungumza mambo mbalimbali ya maendeleo na kutumia nafasi hiyo kuwaalika kwenye ofisi za jiji hilo ili aweze kusikiliza kero zinazo wakabili na kuzipatia ufumbuzi wa haraka.
“Nimefarijika sana leo, kujumuika pamoja kwenye tukio hili muhimu ambalo hutokea kila mwaka , lengo la kuwa na hafla hili , ni kuungana na waumini wote wa dini ya Kiislamu wa jijjni hapa ambao wako katika mwezi mtukufu wa Ramadhani "
"Lakini pia hata wale ambao hawapo kwenye mfungo huu, kupitia hadhara hii tunaweza kukutana na wakazi wengi zaidi na kubadilishana mawazo”.alisema Meya Mwita.
Jiji hili ,linawakazi wengi sana, ambapo huwezi kusema kwamba leo utakwenda kukaa na kila mmoja , lakini yapo matukio ambayo yanatukutanisha kama wanafamilia wa jiji la Dar es Salaam , na hii kwangu ndio faraja zaidi, kutokana tunakutana kwenye matukio ya kiimani, nasio ya ya kisiasa.
Kwa upande wake Sheikh wa Wilaya ya Ilala Adam Mwinyipingu alimpongeza Meya Mwita kwa kuandaa hafla hiyo iliyomkutanisha na baadhya wananchi ambao walishiriki futari hiyo.
Sheikhe Mwinyipingu alisema kuwa jambo hilo ni la heri kwa waumini wote wa kiisilamu na wananchi wote waliohudhuria futari hiyo.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abdallah Mtolea pamoja na mambo mengine alimpongeza meya Mwita kwa kuandaa hafla hiyo, na kusema kuwa imesaidia kuwakutanisha na wananchi wao ambao si rahisi kukutana nao mara kwa mara kutokana
na shughuli zao.
“ Kwa siku ya leo nimeifurahia nimeweza kujumuika na viongozi mbalimbali wa dini, vyama vya kisiasa, na wananchi wa jiji hii ambao tunashindwa kukutana mara kwa mara kutokana na shughuli mbalimbali ambazo wametupatia wananchi ili kuwatumikia.