MCHANGA WA MADINI WAAMIA KWENYE MAGAZETI,SERIKALI JPM YALIFUNGIA GAZETI LA MAWIO ,SOMA HAPO KUJUA
Serikali yalifungia gazeti la Mawio miezi 24 kwa kosa la kuchapisha picha za maraisi wastaafu Benjamini Mkapa na Jakaya Kikwete kwenye toleo lao la leo ukurasa wa mbele kwenye story inayohusu sakata la madini!. Aaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Taarifa iliyotolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Dk Hassan Abbas imesema waziri amechukua hatua hiyo kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 59 cha Sheria ya Huduma za Habari namba 12 ya mwaka 2016.
Amesema hatua hiyo inatokana na gazeti hilo katika toleo namba 196 la 15-21 Juni, 2017 kuchapisha katika ukurasa wa mbele picha za marais wastaafu Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete ikiwahusisha na sakata la mchanga wa madini.
Pia, katika ukurasa wa 12 wa gazeti hilo limechapisha makala iliyoandikwa Lissu: Mkapa, Kikwete wataponaje? Kuwatuhumu viongozi hao kuhusika katika sakata la madini wakati ukweli ni kwamba hawakuwa sehemu ya uchunguzi wa kamati za Rais John Magufuli na wala matokeo ya kamati hizo hayakuwatuhumu kwa kosa lolote.
Taarifa ya Waziri Mwakyembe kwa mhariri mkuu wa gazeti hilo imesisitiza kuwa, licha ya utetezi wao, habari hizo si tu zimekiuka agizo la Serikali lakini pia, zimekiuka vifungu vya 50(a), (b), (c), (d) na (e) vinavyokataza uandishi wenye dhamira hasi.
“Sina budi kulifungia gazeti lako na kukutaka usitishe kulichapisha kwa nakala ngumu au ya mtandaoni kwa kipindi cha muda wa miezi ishirini na nne 24 tangu tarehe ya barua hii kwa mamlaka niliyopewa chini ya sheria ya huduma za habari namba 12 ya mwaka 2016 kifungu 59,” imesema taarifa ya Dk Mwakyembe kwenda kwa mhariri wa Mawio.

Kufungukiwa huku kwa Gazeti la Mawio ambalo ni miongoni mwa Magazeti yanayomilikiwa na Mbunge wa Ubungo,Saed Kubenea inakuja ikiwa ni siku moja kupita baada ya Rais John Magufuli kuvionya vyombo vya habari kuacha kuwahusisha maraisi hao wastaafu na sakata la mikataba na sheria za madini!.
Kwa mujibu ya wanataaluma wa habari, waliozungumza na Fullhabari.blog ambao hawakutaka majina yao yatajwe mtandaoni wamesema hatua ya serikali kulifungia gazeti hilo la wiki ni hatua ya kukurupuka.
Wamesema habari iliyoandikwa kwenye gazeti hilo haikuwahusishwa Marais hao wastaafu.
"ndugu,sahivi ni ubabe tu,yaani hata dunia itatushangaa kweli,yaani unalifungia gazeti kisa picha tu ya marais ,ukisoma habari yenyewe wamezungumziwa hapo ni wakina sumaye na lowassa sasa hawa ni marais wastaafu,maana kamati imewataja mawaziri sasa hawa mawaziri wanaripoti kwa waziri mkuu na waziri mkuu anaripoti kwa rais ,kwahiyo mwandishi kaandika kutokana na vyanzo vyake ,hapa ni kuumiza uhuru wa habaru ambao hawa watawala wanasema wanauenzi"
Hii inakuwa si kwa mara ya kwanza kwa Gazeti hilo kufungiwa na serikali kwani January mwaka jana,Aliyekuwa Waziri wa Habari,sanaa na Michezo,Nape Nnauya alilifungia gazeti hilo kwa mda usiojulikana ambapo mahakama kuu nchini ililifungulia gazeti hilo kwa kile walichokisema Serikali ilikurupuka kulifungia gazeti hilo kwa kujikita hoja ya ''Funga kwanza harafu tutakusikiliza baadae"