BREAKING NEWZZZZ: DAKTARI FEKI ADAKWA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI LEO
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
leo imemtia mbaroni kijana mmoja aliyekuwa akijifanya daktari.
Mtuhumiwa alikuwa akijitambulisha kwa wagonjwa kwamba anaitwa Dk Abdallah
Juma na akijifanya kutoa huduma katika Maabara Kuu.
Uongozi wa hospitali hiyo umesema kuwa kijana huyo
ni daktari feki na si daktari kama alivyokuwa akijitambulisha na kwamba
amekamatwa baada ya kuwekewa mtego na askari wa hospitali hiyo.
Uongozi wa hospitali hiyo umesema kuwa walinzi walikuwa wakimtilia shaka na
kuanza kumfuatilia hadi walipofanikiwa kumkamata.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa
Wateja wa Hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha amesema hospitali imeweka mikakati
mbalimbali ya kupambana na wahalifu wakiwamo watu wanaojiita ni madaktari kama
huyo ambaye amekamatwa leo.
Kulia ni daktari feki ambaye amekuwa
akijitambulisha kwamba ni Dkt, Abdallah Juma ambaye amekuwa akifanya kazi
katika Maabara Kuu, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akiwa chini ya
ulinzi baada ya kukamatwa na mmoja wa askari wa Muhimbili (kushoto).
Daktari feki huyo ambaye amekuwa akijitambulisha
kwamba ni Dkt. Abdallah Juma akiwa chini ya ulinzi