BAVICHA WALAANI KUKAMATWA MEYA WA UKAWA UBUNGO,SOMA HAPO KUJUA
Baraza la Vijana Chadema (Bavicha) limesema litamfungulia kesi Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori kwa kukiuka sheria na kuagiza Meya wa Ubungo, Boniface Jacob awekwe mahabusu.
Mwenyekiti wa Bavicha, Patrobas Katambi amesema vitendo vya wakuu wa wilaya kuagiza kukamatwa kwa viongozi wa Chadema vinaongezeka hivyo hawana budi kuchukua hatua.
Amesema kosa analotuhumiwa Jacob limekuwa likifanywa mara kadhaa na viongozi wa CCM kufanya siasa za chama kwenye majengo ya Serikali.
"Si kweli kwamba meya alikuwa anafanya siasa alitembelewa na viongozi wengine wa Chadema akawa anawaonyesha mazingira yake ya kazi, ghafla likaja agizo akamatwe, tunaomba tabia hii ikome na safari hii tutachukua hatua,"amesema.
Pia Katambi amegusia kukamatwa kwa vigogo wa sakata la Escrow, James Rugemarila na Harbinder Singh na kudai kuwa Bavicha itampongeza Rais John Magufuli endapo vigogo wote waliohusika katika sakata hilo watafikishwa kwenye vyombo vya dola.
BAVICHA WALAANI KUKAMATWA MEYA WA UKAWA UBUNGO,SOMA HAPO KUJUA
Reviewed by Unknown
on
19:24:00
Rating: 5