Zinazobamba

ACT-WAZALENDO YAWANANGA WANAOKIITA CHAMA CHAO KUWA JI CCM B,SOMA HAPO KUJUA

CHAMA Cha Act-Wazalendo Mkoa wa Kagera kimesema kuwa wanasiasa wanaolitumia jina la chama na Kiongozi wa Chama hicho Zitto Kabwe kwa ajenda za Propaganda mbaya wamefeli.

Propaganda hizo ni pamoja na kukihusiha chama hicho na Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja kumtaja na kiongozi kuwa atapewa nafasi kubwa kwenye Serikali ili kukiua chama hicho.

Hayo yamelezwa na Katibu wa Vijana wa Chama hicho Mkoa huo Khalfani Fadhili kupitia ukurasa wake wa mtandao wa picha wa Instergram (@ khalfani_fadhili) ambapo amesema kuwa Chama hicho  hakitarudi nyuma na kwamba hawatayumbishwa na Propaganda za wanasiasa wenye nia ovu na chama hicho.

 Amesema kuwa baadhi ya kauli za wanasiasa kuwa Zitto Kabwe atafungwa na Mdomo kwa kupewa nafasi ndani ya Serikali  kuwa sio za kweli na hazina afya kwenye siasa nchini.
“Zitto sio mmiliki wa  ACT wazalendo bali  ni mwanachama wa  ACT na ni  mbunge mwenye dhamana ya chama pia ni  kiongozi mkuu katika chama.Hivyo ukikuta mwanasiasa mwenye nia ovu  kwa kauli zao za kuwaaminisha watu kuwa Zitto yuko mbioni kupewa Uwaziri ili Act-Wazalendo ife jua huyo  ni mwanasiasa aliyefilisika”
Amesema kuwa wapo wanaowamisha watu kuwa Act-Wazalendo ni sehemu ya CCM ilhali chama cha Act kina sera za kulijenga taifa , ujamaa na uzalendo kwa kushirikiana na watanzania wote bila kujali itikadi zao.

 “Sikatai kuwa haiwezi kuwa akapewa nafasi nyeti katika serikali hii inayoonyesha kuguswa na viongozi wa  ACT.bali nakataa wale wanaolazimisha watu waamini kuwa ACT ni  sehemu ya CCM.Yanaongelewa mengi kuwa Mh.Zitto atafungwa mdomo kwa kupewa nafasi ya juu ili anyamaze.hayo ni  maneno ya chuki dhidi ya chama chetu kwani hata  wao wanazitamani nafasi tulizozipata ACT katika kuilitumikia taifa  hili.”