Chama Cha ACT- Wazalendo kimemtangaza rasmi Mwanasheria Albert Msando kuwa mrithi wa Nafasi ya Mshauri Mkuu wa Chama hicho iliyoachwa awazi na Prof Kitila Mkumbo aliyeteuliwa na Rais Magufuli kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
Msando ambaye ni wakili nchini anatajwa kuwa Rafiki wa karibu wa Kiongozi Mkuu wa Chama hicho,Zitto Kabwe,ambapo mara kwa mara amekuwa akitumika kama mwanasheria wa Kabwe ambaye mbunge wa kigoma Mjini wa Act-wazalendo