CHAMA CHA ADC CHAMUANGUKIA RAIS MAGUFULI,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
CHAMA cha Alliance Democratic Change (ADC)
kimemuomba Rais John Magufuli kubadili agizo lake kwa vyama siasa lakutaka vyama vya siasa nchini kutofanya siasa mpaka 2020 kile alichosema
achwe ajenge nchini ,
Chama cha ADC kimesema agizo hilo litaviangamiza
vyama vya upinzani hasa vichanga kwa madai ya kushindwa kwenda kujiuza kwa
wananchi ili navyo viweze kusikilizwa
sera zao.
Hata hivyo,Chama cha hicho kimetaka utaratibu
utumike katika kuwaondoa katika utumishi wa umma watumishi 9933 ambao inadaiwa
wamefoji vyeti vya kidato cha nne pamoja na vya taaluma ,
Maombi hayo yametolewa leo Jijini Dar es Salaam na
Kamishna Mkuu wa Taifa wa Chama cha (ADC)Doni Mnyamani wakati wa mkutano wa
kuwatambulisha viongozi wa wapya wa manispaa ya temeke wa chama hicho, ambao katika
wilaya hiyo ni mwenyekiti wake ni Asha Mzee huku katibu wake ni Fred John.
Ambapo Mnyamani amesema agizo la Rais Magufuli
kuvizuia vyama vya siasa linakwenda kinyume na sheria ya vyama vya siasa ya
mwaka 1992 ambapo imevipa mamlaka vyama vyote kufanya siasa kwa lengo la
kujijenga.
“Tunamuomba Rais abadili agizo lake ,aturuhusu
tufanye siasa kwani sisi ADC tunashindwa kabisa kujiuza kama vyama vingine
vikubwa,tunabidi twende kwa wananchi ili wananchi watujue sera zetu ili tuweze
kufanya vizuri kwenye changuzi lakini kama agizo hili likiendelea basi
tutashindwa kujilikana kw wananchi,hivyo tunamuomba Rais Magufuli atutazame
tena”Amesema Mnyamani.
Hata hivyo,Mnyamani amezungumzia hatua ya watumishi
waliofoji vyeti huku akitaka busara zitumike.
“Nafahamu wazi kufoji vyeti ni kosa la jina,hivyo
sisi ADC tunaomba busara itumike ya
kuangalia kwa makini hawa watumishi kwani wengi wao wamelitumikia Taifa kwa
kipindi kirefu sana huku baadhi ya wengi wakiwa na familia na watoto
wanawategemea si vema kuwafukuza bila kuwapa hata haki zao za mafao”ameongeza
kusema Mnyamani.