WABUNGE WA UPINZANI WAIGOMA KUISOMA BAJETI YA HII LEO,SOMA HAPO KUJUA
Msemaji wa upinzani katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano, Ally Salehe amesusa kusoma hotuba yake ya upinzani kuhusu wizara hiyo baada ya kulazimishwa kuacha kusoma baadhi ya maneno yakiwamo yanayohusu Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar na mgogoro wa CUF.
Hali hiyo imetokea bungeni leo Jumatatu baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG), George Masaju kusimama na kupinga baadhi ya maneneo aliyotumia kama “Kila wizara imekiona cha moto, wamebanwa mpaka wamevunjwa mbavu” na kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais imeathirika vibaya na kisu cha ngariba kwa kukata bajeti yake.
Baada ya malumbano, Mwenyekiti wa Bunge, Musa Zungu alitoa uamuzi kuwa maneno yaliyoandikwa kuanzia ukurasa wa tatu hadi wa saba kwenye hotuba hiyo yasisomwe wala kurekodiwa kwenye kumbukumbu rasmi za Bunge.
Baada ya uamuzi huo, Salehe alisema basi asingeendea kuisoma hotuba yake na yaliyobaki anamwachia ngariba afanye anavyotaka