Zinazobamba

SERIKALI YA TANZANIA NA SHIRIKA LA KISA KUTOKA KOREA KUSHIRIKIANA KWENYE USALAMA WA MITANDAONI


Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano mapema leo Aprili 19.2017, imetiliana saini ushirikiano katika masuala ya Usalama katika mitandao ya  hapa nchini na Shirika la masuala ya Usalama na Internet kutoka Korea lijulikanao kama  KISA (Korea Internet & Security Agency).
Utiliaji wa saini huo umefanyika Jijini Dar es Salaam ambapo Katibu Mkuu Dkt. Maria Sasabo  alliweza kuiwakilisha Wizara hiyo  na kueleza kuwa, ushirikiano huo utasaidia utendaji wa kazi nakuboresha  maisha  ya kijamii kwa kuwa na usalama na matumizi mazuri ya mitandao.
Dkt. Sasabo amebainisha kuwa, Ushirikiano huo utasaidia kuboresha maisha ya kijamiii na kuwezesha ushiriki wa wananchi wengi katika mifumo yote ya kifedha kwa sababu sasa hivi kila mwananchi mwenye simu ni kama vile amepata benki kwani kuharakisha kupata huduma za kulipa ndipo unapopata unachohitaji hivyo  pamoja na kukuwa kwa teknolojia na faida zake za  uchumi , zimekuja na changamoto za usalama wa mitandao hivyo Serikali  imeamua kushirikiana na Shirika hilo la KISA.
 “Mapema leo kabla ya zoezi hili,  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ameshiriki katika tukio la makubaliano na shirika la KISA ambao ni wataalamu wa mitandao . ushirikiano ambao ni wa kuanzia miaka mitano (5). tutakuwa na mashirikiano ya karibu katika kupata elimu, kubadilishana  wataalamu na pia kuangalia usalama wa miundombinu yetu.
Wenzetu wamepiga hatua zaidi kwenye mawasiliano. kwa mfano simu za Samsung zinatokea Korea kwa hiyo kidogo wametutangulia katika baadhi ya maeneo na tunaangalia uwezekano hata wao kuja kuwekeza baadhi ya viwanda hapa nchini mwetu.” Alieleza  Dk. Sasabo.
Kwa upande wake Rais wa KISA, Bwana.  Oh JinYoung (Jeffrey) ameshukuru Serikali ya Tanzania katika makubaliano hayo ambapo wataendelea kuhimalisha ushirikiano wao katika kufikia malengo.