Zinazobamba

KLABU YA YANGA KUUNG'ANG'ANIA UBINGWA WA LIGI MAHAKAMANI,WABAINI MCHEZO MCHAFU,SOMA HAPO KUJUA

Katibu Mkuu Yanga SC Boniface Mkwasa (kushoto) akiwa pamoja na wajumbe wa kamati ya utendaji Salum Mkemi

Mabingwa watetezi wa Tanzania Bara Yanga SC wamesema hawana imani na kamati iliyoundwa ya saa 72 ya kuchunguza rufaa ya Simba SC kwa Kagera Sugar kwa kuwa imeshaanza mipango ya kuchakachua ripoti ya mwamuzi kwa lengo la kusaka ushindi wa mezani.

Hayo yameibuliwa na Katibu Mkuu wa Yanga SC pamoja na wajumbe wa kamati yake ya utendaji ikiongozwa na Salum Mkemi kwa kusema haitakuwa jambo la rahisi kwa kupata haki ya ukweli kwa kile kinachoonekana ndani ya kamati hiyo kujaa maslahi binafsi badala ya kulinda heshima ya ligi.

"Kamati hii imechelewa kutoa maamuzi kwa kuandaa ripoti za uongo za michezo dhidi ya Fakhi pia tuna taarifa za kughushiwa barua pepe (email) na nyaraka nyingine, ili kuipa alama tatu Simba SC yenye zaidi ya wajumbe 6 ndani ya kamati hiyo. Tumeshavijulisha vyombo husika yaani TAKUKURU na watu wa 'Cyber Crime' na TCRA juu ya uchunguzi wa mawasilano ya waamuzi wote waliohusika na kutajwa kwenye rufaa hiyo". Alisema Mkemi pindi alipokuwa anaongea na wanahabari katika ukumbi wa klabu hiyo, Jangwani jijini Dar es Salaam
Vile vile mjumbe huyo ameendelea kubainisha baadhi ya vitu kwa kusema wameshaanza kufanya uchunguzi wao na kutoa taarifa kwa vyombo vya dola huku wakijipanga kwenda mahakamani endapo wapinzani wao watabebwa kwa namna moja ama nyingine.

"Kama Yanga tumeanza uchunguzi wetu na kutoa taarifa kwa vyombo husika vya dola pia maamuzi yoyote ya kuibeba Simba tutakwenda mahakamani licha ya sheria za FIFA kukataza hivyo kama hawataki tufike huko lazima haki itendeke". Amesisitiza Mkemi
Hata hivyo klabu hiyo imetoa rai yao kuwa ifike wakati ziundwe kamati zisizokuwa na maslahi pande yoyote ile ili kuleta haki katika maamuzi mbalimbali y soka nchini.

Kwa upande mwingine imewapongeza timu ya Simba SC kwa ushindi wao wa jana dhidi ya Mbao FC kwa kuonesha kupambana na kuweza kurudisha wao.