SERIKALI YAWASHUKIA MAAFISA ELIMU NCHINI,YAWAPA SIKU 30,SOMA HAPO KUJUA
Serikali imetoa siku 30 kwa maofisa elimu wa mikoa na wilaya zote nchini kuhakikisha wamelipa madeni yote yanayohusu uhamisho wa walimu huku ikipiga marufuku kuanzia sasa kufanyika uhamisho kiholela kwani kunazalisha madeni yasiyo ya lazima ambayo yanachangia kuwepo kwa migogoro isiyoisha kati ya serikali na watumishi wa kada hiyo.
Kauli hiyo ya serikali inatolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Mhe George Simbachawene wakati akizungumza na maofisa wa elimu wa mikoa na wilaya zote mjini Dodoma ambapo amesema uhamisho usio wa lazima ni kukiuka waraka uliotolewa na serikali wa kutozalisha madeni yasiyo ya lazima ambayo malipo yake hayajaidhinishwa na mamlaka yeyote.
Aidha Waziri Simbachawene amekiri sekta ya elimu inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemoupungufu mkubwa wa madarasa ambapo kwa shule za msingi kuna mahitaji ya madarasa zaidi ya 127000 na madarasa 10200 kwa sekondari huku akizitaka mamlaka za serikali za mitaa kuendelea na utaratibu wa kuwashirikisha wananchi na wadau kuchangia nguvu na fedha kwa ajili ya ujenzi kwani serikali peke yake haiwezi kutatua.
Awali Maofisa elimu hao walimueleza waziri changamoto mbalimbali zinazowakabili katika utendaji wa o wa kila siku ikiwemo uhaba wa vitendea kazi yakiwemo magari kwa ajili ya kutembelea mashule kwa ajili ya ukaguzi,bajeti ndogo ya fedha za kuendeshea ofisi pamoja na kuingiliwa katika majukumu yao na baadhi ya viongozi na wanasiasa hali inayochangia walimu kuzembea na kiwango cha utoaji elimu kushuka