Zinazobamba

CHADEMA YACHUKIZWA NA KUFUKUZWA KWA NAPE UWAZIRI NA KUTISHIWA BASTOLA,SOMA HAPO KUJUA


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo Bara (Chadema) leo kimelaani kitendo cha vyombo vya dola kutumia vibaya silaha ya moto iliyotolewa na askari kanzu mmoja jana dhidi ya aliyekuwa Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, wakati akitaka kuzungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam.

Hayo yalisemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, leo wakati akitangaza majina mawili yaliyoteuliwa kupitia kamati kuu ya chama hicho iliyokaa kwa muda wa siku mbili hadi jana ambao ni Ezekiel Wenje na Lawrence Marsha ambao watagombea ubunge wa  Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Pia alilaani kitendo cha uvamizi kilichofanywa katika kituo cha redio na televisheni cha Clouds jijini Dar es Salaam ambapo askari waliingia wakiwa na silaha za moto.

Alisema  katika nafasi za kugombea ubunge wa jumuiya hiyo chama tawala (CCM) kina nafasi sita wakati Chadema kina nafasi mbili na Chama cha Wananchi (CUF) nafasi 1.  Jumla ya nafasi za wabunge wa jumuiyahiyo ni tisa.