MWEKEZAJI YUSUFU MANJI BADO ANAWEWESEKA,MAWAKILI WAKE WAKIMBILIA MAHAKAMANI,SOMA HAPO KUJUA
Mfanyabiashara
maarufu Yusuf Manji amewasilisha hati ya kuiomba Mahakama Kuu iwaagize
maofisa Uhamiaji wamfikishe mahakamani ili kesi yake isikilizwe kwa
mujibu wa sheria.
Manji
yuko kwenye matibabu Hospitali ya Aga Khan jiji hapa akiwa chini ya
ulinzi baada ya kuachiwa kwa dhamana. Februari 20 mwaka huu, alipelekwa
ofisi ya Uhamiaji mkoa na kuhojiwa kwa madai ya kuingia nchini kinyume
cha sheria.
Katika
kesi hiyo wajibu maombi hayo ni Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Ofisa
Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG) na
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.
Wakili
wa Manji, Hudson Ndusyepo aliyefungua kesi ya maombi hayo, anataka
Mahakama iagize maofisa uhamiaji na polisi kumfikisha mahakamani ili
iamue uhalali wa kushikiliwa kwake na kuagiza aachiwe.
Katika
hati ya maombi hayo, Ndusyepo anadai kuwa alimtembelea mteja wake
hospitali ya Aga Khan Februari 17 mwaka huu na kukuta maofisa wa
Uhamiaji wakimsubiri mteja wake wampeleke kwa ofisa Uhamiaji wa mkoa kwa
mahojiano dhidi ya tuhuma kuwa siyo raia wa Tanzania.
Kwa
mujibu wa Ndusyepo, Manji ambaye ni Mwenyekiti wa Quality Group Limited
na Diwani wa Mbagala Kuu, Amedai kuwa alitoa maelezo kwa maofisa
Uhamiaji na alirudishwa Aga Khan ambako yupo chini ya ulinzi hadi leo.