DK MWAKYEMBE AUMBULIWA VIBAYA,HASHIM RUNGWE AMTAKA AFUNGE MDOMO,SOMA HAPO KUJUA
Mwenyekiti
wa CHAUMMA, Hashim Rungwe amemtaka Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.
Harrison Mwakyembe kuacha kuingilia mambo yanayohusu chama cha
wanasheria Tanganyika (TLS) hasa kwenye suala uchaguzi wa kumsaka Rais
wa chama hicho
Akijibu
maswali ya wananchi kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa katika
ukurasa wa Facebook EATV, Mh. Rungwe amesema kuwa TLS ina utaratibu wake
wa kuendeshwa na kamwe haiwezi kupelekwa kama jinsi waziri anavyotaka
kwani chama hicho kinaongozwa kwa sheria na kanuni.
“Yeye
kama Waziri maoni yake ni muhimu, lakini anasema vijana hawa wawili
wana maoni ya kisiasa yaani Lissu na mwenzake lakini wakati huo huo yeye
ni waziri na mpaka amefika hapo yupo ndani ya chama cha kisiasa. na
amevaa kofia mbili. TLS haiwezi kuendeshwa kama anavyotaka yeye, huwezi
kutengeneza utaratibu nje ya utaratibu. Tuheshimu pia taaluma za watu."
Rungwe alifunguka.
Aidha
Rungwe ambaye pia ni Wakili wa Mahakama Kuu na Mwanachama wa chama
hicho ameongeza kuwa katika chama hicho hakuna sheria ambayo inamzuia
mwanasiasa yoyote kugombea nafasi na kuongeza kwamba kuwazuia upinzani
wakati waliomo kwenye chama tawala wanaruhusiwa ni kutengeneza chuki
ndani ya jamii na nchi kwa ujumla
"Kutengeneza
chuki kwa makusudi it's a great crime, hasa chuki ikitengenezwa na
viongozi waliopo madarakani, ambao wamepewa dhamana ya kuwaongoza
wananchi yeye atuache na TLS yetu, kama itaonesha watu hawa hawaruhusiwi
kugombea basi watazuiliwa kwasababu watu wanaochuja wagombea ni sisi
wenyewe". Amesema
Hivi
karibuni Waziri huyo wa Sheria na Katiba alinukuliwa akisema kuwa
serikali haiwezi kuona (TLS) ikinajiingiza katika siasa na kuongeza kuwa
kama wanataka hivyo, basi serikali haitasita kuifuta Sheria ya TLS Sura
ya 307 iliyoanzisha chama hicho cha wanasheria.