Zinazobamba

BENKI YA DCB YAZIDI KUWAJALI WATEJA WAKE,YAJIPANGA KUFANYA HIVI KWA MWAKA HUU,SOMA HAPO KUJUA



Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya DCB,Edmund Mkwawa 
NA KAROLI VINSENT
Imeelezwa kuwa moja ya kipaumbele cha benki ya DCB kwa mwaka huu nikutoa huduma ya mikopo kwa vikundi kwakuwa ndio chimbuko kuu la kuanzishwa kwake.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Edmund Mkwawa mwishoni mwa wiki  wakati wa hafla ya utaoji zawadi kwa tawi la Magomeni ambalo ndio
mshindi wa huduma za Vikundi kwa wateja wake, ambapo amesema kuwa huduma hiyo imelenga zaidi kuwa hudumia wajasiriamali wadogo ili kuinua Maisha yao.

"Kama mnavyojua huduma hii ni chimbuko kuu la kuanzishwa kwa DCB ikilenga zaidi kuwahudumia wajasiriamali wadogo ambao walikuwa hawapati huduma za kifedha kwenye mabenki makubwa ili kuinua hali ya Maisha yao". Alisema Mkwawa

Mkwawa amewapongeza washindi na kuwakumbusha kuwa mafanikio yoyote yanatokana na uongozi imara na kuwataka wengine kuiga mfano na kujituma maradufu ili kuongeza mafanikio ya taasisi hasa katika kipindi hiki ambapo biashara imekuwa ngumu.

Kwa Upande wake mgeni rasmi ambaye ni Makamu mwenyekiti wa Bodi Prof. Lucian Msambichaka amesema kuwa hayo ndio mambo ambayo bodi yake inahitaji kuyaona kutoka kwa wafanyakazi matawi mbalimbali kwani ushindi huo unatakiwa kuchukuliwa kama changamoto kwa wafanyakazi ili kuendeleza wimbi la ushindani ili kuongeza ubunifu na maarifa ya hali ya juu katika kutafuta na kupata biashara kutoka kwa wateja.