SERIKALI YAWATOA HUFU WANANCHI KUHUSU UGONJWA WA ZIKA,SOMA HAPO KUJUA
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto imekanusha uwepo wa taarifa juu ya ugonjwa wa ZIKA hapa
nchini.
Waziri wa Afya, Mh. Ummy Mwalimu pamoja na Naibu
wake Dk. Hamisi Kigwangalla wakitolea ufafanuzi mbele ya waandishi wa Habari,
wamesema wananchi wasiogope na wamewatoa hofu kwani taarifa zilizotolewa awali
na kuripotiwa na vyombo vya habari walizonukuu kutoka NIMR hazina ukweli wowote
na za kupuuzwa.
Aidha, kwa mujibu wa Kaimu Mkuu kitengo cha
Mawasiliano Serikalini (Afya), Bi. Catherine Sungurakatika taarifa ya Waziri wa
Afya, Mh. Ummy Mwalimu ilieleza: “Napenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa
zilizoenea kwenye vyombo vya habari na mitandao ya jamii kuhusu uwepo wa
ugonjwa wa Zika nchini.
Kama nilivyoeleza mnamo tarehe 31 Januari 2016,
ugonjwa huu bado haujaingia nchini, na leo pia napenda kuwatoa hofu wananchi
kuwa kwa sasa Tanzania haujathibitishwa kuwepo na ugonjwa wa Zika. Utafiti
uliofanywa na NIMR, ulikuwa ni utafiti uliofanyika nchini wa kuchunguza ubora
wa kipimo kipya cha kupima magonjwa ya zika na chikungunya.
Kwa utaratibu wa kitafiti, hii ni hatua ya
awali tu ya kuangalia ubora na uwezo wa kipimo hicho.Matokeo haya bado
yanahitaji kuchunguzwa kwa kina zaidi kupitia vipimo vilivyothibitishwa na
Shirika la Afya Duniani.
Wizara itaendelea kushirikiana na Taasisi mbalimbali
mbali ndani na nje ya nchi kuendelea na utafiti na ufuatiliaji wa kitaalamu ili
kuzuia ugonjwa huu kuwepo Tanzania. Ufuatiliaji wa magonjwa ni endelevu katika
sekta ya afya na tuna taratibu za utoaji taarifa wa magonjwa ya kuambukiza na
hatari kama vile zika, ebola na mengineyo. Wizara yangu imeshaandaa mkakati wa
Zika nchini, ambao unaelekeza utelezaji wa ufuatiliaji wa Zika.
Post Comment