MAWAZIRI WA MAGUFULI WAZIDI MIMINIKA OFISI ZA WASAFI,BAADA YA NAPE,MAKAMBA,WAZIRI HUYU NAYE ATINGA,SOMA HAPO KUJUA
Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba
wiki hii alitembelea ofisi ya WCB iliyopo Sinza Mapambano jiji Dar es salaam na
kujionea uwekezaji uliofanywa na label hiyo ambayo ipo chini ya Diamond
Platnumz.
Waziri huyo kijana aliweza kuzungumza na viongozi wa
label hiyo na kuangalia namna ambavyo serikali inaweza kudhibiti wizi wa kazi
za wasanii.
Baada ya kumaliza mazungumza hayo, Waziri Nchemba
kupitia instagram yake aliandika:
#Wizi wa kazi za
wasanii #Jeshi la polisi kuongeza nguvu
Pia alisema kuwa serikali haitasita kuwapa msaada
pale watakapokwama na kuhitaji usaidizi wa serikali.