Hata
hivyo Mkurugenzi huyo ameipongeza serikali kwa kufanya mabadiliko ya
msingi katika kupunguza rushwa na ubadhilifu serikalini japo kuwa bado
kuna ukandamizwaji unaotokana na sheria mpya zinazoleta vikwazo vipya
kwenye haki ya kujieleza na mchakato wa utungaji wa sheria Huduma za
vyombo vya habari.
Ikumbukwe
kwamba kila tareh,10 ya Mwezi huu wa 12 kila mwaka tangu mwaka 1950
imekuwa ni siku maalumu ya haki za binadamu kimataifa, na tangu
kusajiliwa kwa kituo hiki mwaka 1995 wamekua wakiadhimisha siku hii kwa
kufanya shughuli mbali mbali ili kuinua juu ajenda ya haki za binadamu.