HOSPITALI YA AGAKHAN YAWAJALI WATANZANIA,SASA WAJA NA KITU MUHIMU,SOMA HAPO KUJUA

Wanawake na watoto nchini waliopata majeraha ama
makovu kwenye miili yao hospitali ya Agakhan ili waweze kufanyiwa upasuaji wa
kurekebisha viungo vyao viweze kuwa katika hali ya awali.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
salaam mwakilishi kutoka wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na
watoto Dk. Ally Sadiki amesema kuwa upasuaji huo utafanywa kwa ushirikiano
wa hospitali ya taifa ya muhimbili ambapo maatibabu ya kurekebisha viungo ya
tadumu kwa kipindi cha miaka miwili.
Amebainisha kuwa kuwepo kwa huduma hiyo ni moja ya
mikakati ya Serikali ya kuhakikisha inahudumia wananchi wake hasa wale
wasiokuwa na uwezo wa kumudu gharama za matibabu na kuongeza kuwa ni vizuri
wananchi wakashiriki kupata huduma hiyo.
Naye muuguzi kiongozi idara ya upasuaji kutoka
katika hospitali ya Agakhan Zainabu Mallya ameeleza kuwa huduma hiyo inatolewa
mahususi kwa watoto na wanawake kwa kuwa wao ndiyo kundi kubwa la watu
wanaopata ulemavu wa viungo kutokana na manyanyaso ya kijinsia na matibabu yote
yatatolewa bure bila gharama.