Zinazobamba

SIRI YAFICHUKA YA SERIKALI KUMPORA SHAMBA SUMAYE,KUMBE YALIYOMKUTA MBOWE, LOWASSA NA KUBENEA YATAJAWA KWA SUMAYE,SOMA HAPO KUJUA

NA KAROLI VINSENT
WAKATI Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Joh Magufuli ikiwa ni kama imezamilia kuwakomoa vigogo wa Upinzani,baada ya serikali hiyo ikiwa teyari imeshamfukuza kwenye nyumba ya shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema,Freeman Mbowe kwa kile  inachokidai mwenyekiti huyo ameshindwa kulipa kodi ya pango katika jengo.

Na baadae serikali hiyo inayojiita  "serikali ya Hapa kazi” pia ikawa pia imekifungia kituo cha Redio Five cha Arusha ambacho kinamilikiwa na Waziri mkuu wa Zamani  ambaye alikuwa mgombea wa Urais wa Chadema kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana,Edward lowassa kwa kile inachosema serikali  hiyo kuwa kituo hicho kimerusha taarifa za uchochezi.
Mbali na Lowassa,serikali hiyo ikiwa imeyafungia Magazeti ya Mawio,Mseto ambayo yanamilikiwa na Mbunge wa jimbo la Ubungo (CHADEMA),Saed Kubenea kwa hoja ya magazeti hayo yanaandika habari za uchochezi.

Sasa ni kama zahama  kama hayo ya hapo juu. yamemkuta pia Waziri mkuu Mstaafu wa awamu ya tatu,Fredrick Sumaye  ambaye alikuwa ni mmoja wa wasemaji tegemeo katika mikutano ya kampeni ya Uchaguzi Mkuu uliopita ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Baada ya Rais Magufuli kumnyang’anya  shamba lake lenye ukubwa wa hekta 33 kwa kile kilichoelezwa kushindwa kuliendeleza.


Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amesema kuwa Serikali imefikia uamuzi huo baada ya Sumaye kushindwa kuliendeleza kama notisi ya siku 90 ilivyoeleza.

“Oktoba 28, mwaka huu. Rais John Magufuli alibatilisha hati ya kumiliki ardhi ya shamba namba 3074 lililopo Mabwepande. Shamba hili lilikuwa na hati namba 53086. Jina la mmiliki lililoandikwa katika hati ni Frankline Sumaye,” amesema Hapi.

Akizungumzia hali hiyo Kigogo kutoka ndani ya serikali Aliyejiiita kuwa  anamapenzi mema na upinzani wa nchi hii huku pia hakutaka jina lake litajwe mtandaoni aliumbia mtandao wa  ‘Fullhabari.blogs” hatua hiyo inalengo la kumnyamazisha Waziri mkuu huyo ambaye anaushawishi mkubwa nchini na ambaye anatajwa uwenda ni mtu hatari kwenye uchaguzi wa Mwaka 2020.

“Tatizo jeraha la uchaguzi wa mwaka jana linawatesa viongozi wa nchi hii,hivi hoja la sumaye kutoliendeleza shamba ziko wazi ni kwamba kuna kesi mahakamani,sema viongozi hawa wanauoga na sumaye kuelekea uchaguzi wa mwaka 2020,wanajua sahav hali ya nchi mbaya hakuna ajira mpya,wanafunzi hawa mikopo,uchumi upo vibaya,mabenk yanafirisika,umasikini umeongezeka”:

“Kwani kuna vigogo wangapi ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM,wanamashamba na wameshindwa kuyaendeleza,leo wanamuona Sumaye tu,nakwambia hawa watawala wanauoga ndugu,"kimesema Chanzo chetu hicho.