MBUNGE LEMA KESI YAKE YAZIDI KUWA NGUMU,MAHAKAMA YAENDELEA KUMNYIMA DHAMANA,SOMA HAPO KUJUA
Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema amekwaa kisiki
kwa mara nyingine katika harakati za kuomba dhamana baada ya Mahakama Kuu Kanda
ya Arusha kutupilia mbali ombi la marejeo ya kesi yake na kushauri kuwa
Mawakili wake wakate rufaa ya kupinga zuio la dhamana
Mawakili wa Lema leo walikuwa wakirusha karata hiyo
kwa mara ya tatu baada ya mara mbili za awali mteja wao kushindwa kupata
dhamana.
Lema amesota rumande tangu alipokamatwa Novemba 3,
2016 akiwa mkoani Dodoma na kusafirishwa hadi Arusha ambapo anashtakiwa kwa
kosa la uchochezi dhidi ya Rais Dkt Magufuli.