ZITTO KABWE AJITOSA UGOMVI KATI YA LEMA NA RC GAMBO,AAMUA KUWATOLEA UVIVU,SOMA HAPO KUJUA
Jana October 18 2016 kulifanyika hafla ya
uwekaji wa jiwe
la msingi katika hospitali ya mama na mtoto inayojengwa eneo ya
Burka nje kidogo ya jiji la Arusha, lakini shughuli hiyo ilisimama baada
mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kusimama kupinga maelezo
yaliyokuwa yakitolewa na mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.
Maelezo ya RC Gambo yalisema kwamba eneo la mradi
ule limetokana na maono aliyokuwa nayo Marehemu Advocate Nyaga Mawala, maelezo
ambayo mbunge Lema alikuwa akiyapinga na kudai yeye amehusika kutafuta ardhi na
wafadhili, Lema alidai maelezo hayo yamejaa upotoshwaji na siasa ndani. Unaweza
kuangalia video hii hapa chini.
Leo October 19 2016, mbunge wa kigoma mjini na
kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa
facebook ametoa ushauri kwa RC Gambo na Mbunge Lema, Zitto amesema…..…
"Nakasirishwa sana kuona viongozi
vijana wanafanya mambo ya hovyo. Mkuu wa mkoa wa Arusha mdogo wangu Mrisho Gambo
una dhamana zaidi Kwa vijana. Mnapofanya mambo ya kijinga mnaharibu nafasi ya
vijana kuaminiwa zaidi.
"Kaa Na Mbunge Godbless Lema
mnywe kahawa pale New Arusha Na muanze upya. Ndugu yangu Lema nashauri punguza
munkari. Juhudi zako Arusha haziwezi kufutika kirahisi.
"Nakushauri kaa chini Na Mkuu wa
Mkoa wako mpige mstari muanze Kazi upya Kwa pamoja. Viongozi jiepusheni
kuonyesha hasira zenu hadharani. Sio hekima."-Zitto
Kabwe