SUALA LA AJIRA MPYA SERIKALINI LAGEUKA KUWA SINEMA,SERIKALI YAJA NA HILI LEO
1.Ipo taarifa inayosambaa katika mitandao ya kijamii
ikimnukuu Waziri wa Nchi -Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora) Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb), kuwa Serikali itaanza kutoa ajira,
kupandisha Vyeo na kulipa Stahiki mbalimbali za Watumishi wa Umma mwezi
Februari, 2017. Chanzo cha habari hiyo ni mtandao wa Jamii Forum kupitia
mjadala ulioanzishwa na nkanga chief (JF-Expert Member) na baadaye
kusambazwa katika mitandao mingine.
2. Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora inapenda kuwafahamisha Watumishi wa Umma na Umma kwa ujumla kuwa,
taarifa hiyo haina ukweli wowote na ina lengo la kuupotosha
Umma. Hivyo watumishi wa umma na wananchi kwa ujumla
wanaombwa kuipuuza taarifa hiyo na kuendelea na majukumu yao kama kawaida.
3.Serikali inasisitiza kuwa, suala la Ajira mpya na
upandishaji Vyeo litafanyika kwa kuzingatia Bajeti ya Serikali ya Mwaka wa
Fedha 2016/17. Malipo ya stahili za watumishi wa umma yatafanywa na Serikali
kwa kuzingatia, Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo.
4. Ikumbukwe, Serikali ina utaratibu maalum wa kutoa
taarifa kwa Umma, hivyo Serikali itatoa taarifa rasmi kwa Umma kupitia mamlaka
husika.
5. Serikali kupitia taarifa hii inawaasa wananchi
kuacha tabia ya kusambaza habari za uongo au zisizothibitishwa dhidi yake.
Serikali haitasita kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika
kuzusha na kusambaza habari za upotoshaji kuhusu shughuli za Serikali.
Imetolewa na: