TCRA YAIFUNGULIA MAGIC FM REDIO .PIA YAENDELEA KUING'ANG'ANIA REDIO YA LOWASSA,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Meneja mipango wa Kituo cha Redio Magic Fm orest Kawau ambaye ni miongoni mwa watangazaji wa kipindi cha Morning Magic picha na Maktaba |
KAMATI ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasilioni nchini (TCRA)
Imekifungulia Kituo cha Redio cha Magic
Fm cha DaresSalaam na kuhiruhusu
kuendelea na matangazo yake pamoja na kuiipa onyo kali.
Hata Hivyo,Kamati hiyo imekifungia kwa miezi mitatu
pamoja na kuitoza faini ya milioni 5 kituo cha Redio Five cha Mkoani Arusha
kituo hicho ambacho kinamilikiwa na Waziri Mkuu wa Zamani,Edward Lowassa.
Akitoa hukumu hiyo leo Jijini dare s Salaam,Mwenyekiti
wa Kamati hiyo,Joseph Mapunda amesema Mamlaka hiyo imetoa hukumu hiyo baada ya
kujilidhisha pande zote mbili.
Mapunda, amesemakuwa kituo Redio Five kilirusha maneno yaliyo
tamkwa na Lema ambayo yalikuwa yakihamasisha wananchi kushiriki katika
maandamano ya Ukuta yaliyopigwa marufuku na Jeshi la Polisi.
“Maneno ya Lema yalilenga kuhaasisha wananchi kupambana na jeshi
la polisi na hivyo kusababisha uvunjif
u wa amani na kuhatarisha usalama wa
Taifa,” amesema.
Mapunda amesema uamuzi huo umetolewa na kamati hiyo baada ya
kamati hiyo kusikiliza maelezo ya utetezi yaliyotolewa na wa Uongozi wa Redio 5
Arusha.
“Baada ya kusikiliza maelezo ya utetezi kamati imeridhia kuwa
kipindi cha matukio kilikiuka baadhi ya kanuni za maudhui namba 5(a,b,c,d,f,h)
6(2) (b, c) na 18 (1) (b),” amesema.
Ameongeza kuwa ” kituo hicho kinatozwa faini ya sh. Milioni 5
ambazo zitatakiwa kulipwa ndani ya siku 30 kuanzia leo, kinafungiwa kwa miezi 3
na kuwekwa chini ya uangalizi maalumu kwa muda wa Mwaka 1 baada ya kipindi cha
kufungiwa kumalizika, “
Hata hivyo, Mapunda amesema haki ya wahusika kukata rufaa dhidi ya
uamuzi huo iko wazi ndani ya siku 30 kuanzia leo.
Kwa upande wa kituo cha redio cha Magic Fm ambacho nacho pia kwa
mujibu wa kamati hiyo kinadaiwa kukiuka kanuni za maudhui kupitia kipindi chake
cha Morning Magic kipengele cha Paka Rangi ambapo kilirusha maneno yanayodaiwa
kumkejeli rais na wananchi, kimepewa onyo kali pamoja na kutakiwa kuomba radhi
kwa muda wa siku tatu mfululizo.
“Baada ya kusikiliza na kutafakari kwa kina maelezo ya utetezi
yaliyotolewa na Uongozi wa Magic Fm Redio, Kamati ya Maudhui imeridhika kuwa
kipindi cha Morning Magic kilikiuka baadhi ya kanuni za huduma za utangazaji
2005. Kamati ya maudhui inaamua kutoa onyo kali kwa Magic Radio, ” amesema na
kuongeza.
“Pia inatakiwa kumuomba radhi Rais John Magufuli, wasikilizaji na
wananchi kwa ujumla. Tangazo la kuomba radhi litolewe kwa siku tatu mfululizo
katika taarifa za habari za saa 10.00 alasriri, na 3.00 usiku kuanzia tarehe
17,9,2016.”
Vituo hivyo ambavyo vilifungiwa na waziri wa
Habari,utamaduni,sanaa na Michezo,Nape Nnauya kwa madai kuwa vituo hivyo kwa
madai ya kutoa taarifa za uchochezi.
Waziri Nape alidai kuwa kwa Mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 28(1)
cha sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ya mwaka 2003 imempa
mamlaka ya kuvifungia vituo hivyo,
Amesema Uamunuzi wa kuvifungia vituo amefikia baada
kujiridhisha kuwa Redio five katika kipindi cha matukio kilichorushwa tarehe 25 Agosti,2016 muda wa saa 2;00 usiku
hadi saa 3;00 usiku ambapo katika
kipindi hicho alimuhojiwa Mbunge wa Arusha Majini,Godbless Lema ambapo alikuwa
anatoa maneno anayosema ni uchochezi.
Amesema licha ya Mbunge huyo kutoa lugha hizo,lakini
watangazaji wa kipindi hicho walishindwa kumsahihisha jambo analodai linakwenda
kinyume na sheria ya utangazaji.
Mbali na Redio hiyo inayomilikiwa na Lowassa ambaye
ni Alikuwa ni mgombea wa Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Chadema kwenye uchaguzi uliopita pia ametaja kosa lilipelekea kukifungia kituo
cha Magic Fm cha Dar es Salaam.
Amedai mnamo tarehe 17,Agosti 2016 katika kipindi cha
Morning Magic kipindi hicho kilichoruka
mda saa 1.00 asubuhi na saa 2.30 katika kipengele cha Kupanga
Rangi watangazaji wa kipindi hicho walisikiaka wakitoa maneno anayoeleza kuwa
ni ya uchochezi.
“Watangazaji hawa Magic walisema kama Rais anavunja
Katiba sasa wananchi wa chini wafanyaje,nao lazima watafanya hivyo,”Amesema
Nape.
Waziri Nape alidai kuwa
Endelea kufuatilia Fullhabari.bllogs habari kamili
utapa