WANAFUNZI "VILAZA" WA MAGUFULI WAIBURUZA SERIKALI MAHAKAMANI,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
WAKATI serikali chini ikiwa imeshikilia kauli yake
kuwa wanafunzi 480 waliofukuzwa katika chuo kikuu cha Mtakatifu Joseph ni “vilaza”
na hawana sifa ya kudahiliwa kwenye chuo kikuu nchini ,
Nao wanafunzi hao wameibuka na kuishtaki Tume ya
Vyuo vikuu nchini (TCU) mahakamani kwa hatua ya kuwaruhusu wanafunzi hao
kujiuunga na chuo kikuu wakati wakiwa hawana sifa.
Mbali na (TCU)
pia wanafunzi hao wamekishtaki Chuo kikuu cha Mtakatifu Joseph kwa hatua yake ya kuchukua ada za masomo wanafunzi hao huku
wakijua hawana sifa za kusoma chuo kikuu.
Licha kukistaki chuo hicho pia wameitaka mahakama
kuzuia mara moja masomo yote yanayoendelea katika chuo hicho mpaka haki yao ya
msingi itakaposikilizwa na mahakama.
Akithibitishwa kufunguliwa kwa kesi huyo,Emmanual
Muga ambaye ni wakili kutoka kampuni ya Agustino Law Office amewaambia
waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, kuwa kesi hiyo imefunguliwa kwenye Mahakama kuu kanda ya
Dar es Salaam na kupangiwa kusikilizwa na Jaji wa mahakama hiyo Elieza
Felishi.
Wakili Muga amesema kesi hiyo ya namba 311 ya mwaka 2016
inatarajiwa kuanza kutajwa kesho ambapo wanafunzi 316 kati ya 480 ya
waliofukuzwa ndio wamefungua kesi wakitaka haki ya sheria ingilia kati maamuzi
yaliyofanywa na Serikali.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni