SHEIKH JALALA :RAMADHANI YA MWAKA HUU IWE DARASA LA HURUMA NA UPENDO
Kiongozi Mkuu wa chuo cha Kiislamu(HAWZA) Immam Swadiq
Sheikh Hemed Jalala amewataka Waislamu na wasiokuwa waislamu kuitumia fursa ya
mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuachana na matendo yasiyompendeza Mungu na badala
yake wajikite katika kuoneana huruma na kupendana miongoni mwao kwani kufanya
hvyo ndiyo Mafundisho ya Mtume.
Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake, Kigogo Jijini Daresalaam wakati wa tukio la kuukaribuisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Sheikh Hemed Jalala amesema Mwezi wa Ramadhani unamafundisho mengi lakini kubwa watu wanapaswa kuoneana huruma na kupendana
Amesema licha ya Ramadhani kuwa na Mafundisho mengi, kwa
mwaka huu Jamii haina budi kuhakikisha wanaitumia Ramadhani kwa kuwaonea huruma
wazee, mayatima, vikongwe na majirani zao kwani kufanya hivyo kutaongeza ustawi
wa Amani miongoni mwa jamii.
“Funga ya mwaka huu naomba nifikishe ujumbe kuwa iwe ni darsa la kuwahurumia mafakiri, mayatima
na majirani zao nah ii ni kwa wote wawe Waislamu na wasio Waislamu, Wote
tunajua anayefunga anaacha chakula chake anachopenda ili kuungana katika
Ramadhani….ni somo la kufahamu mengi kuhusu wenzetu mafakiri, mayatima na
wajane wanayopitia” Alisema Sheikh Jalala.
Katika hatua nyingine, wakati Nchi ikiwa katika sintofahamau kubwa kutokana na matukio ya mauaji ambayo yameitikisa
nchi kwa kipindi kifupi na kuacha watanzania wakiwa katika wasiwasi Sheikh Jalala ametumia fursa hiyo kulaani vikali mauaji ambayo
ameyaita ya kiigaidi yaliyotokea katika mikoa mbalimbali nchini huku akisema
kuwa vitendo hivyo vinakwenda kinyume na Imani ya dini yoyote nchini na vinastahili
kupingwa na kila mtanzania.
Sheikh JALALA amesema kuwa
Tanzania ni nchi iliyotambulika duniani kote kuwa kisiwa ya Amani na utulivu hivyo vitendo hivyo ni
vitendo ambavyo vinaharibu sifa ya nchi duniani kote.
Ameongeza kuwa vitendo
vya ugaidi na ukatili pamoja na uvunjifu wa Amani nchini ni vitu vya kuwa
makini sana na kuwa na tahadhari sana kwani vinaweza kuzuia hata waumini
mbalimbali kuabudu kwa uhuru na Amani hasa kipindi hiku cha mfungo
Aidha amewataka
watanzania sasa kuchukua jukumu la kuwa walinzi wa maeneo wanayoishi na
kuhakikisha kuwa wanatoa taarifa haraka pale ambapo wanaona watu au kikundi cha
watu ambao hawaeleweki wakiwa katika maeneo yao huku akivitaka vyombo vya
usalama kuhakikisha kuwa wanachukua taarifa za wananchi na kuzifanyia kazi mara
moja ili kuepuka kutokea kwa matukio ya kigaidi na mauaji kama yaliyotokea
mwezi huu.
Tukumbuke kuwa siku za
hivi karibuni kumekuwa na mfululizo wa matukio ya mauaji ya kutisha huku
wengine wakichinjwa ambayo yaiyokea mkoani mwanza na mengine mkoani tanga
matukio ambayo yameacha simanzi kwa watanzania walio wengi.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni