MKAPA AANZA KUYAJUTIA ALIYOYAFANYA IKULU,SOMA HAPO KUJUA
RAIS Mstaafu, Benjamin Mkapa haachi
kujuta kutokana na baadhi ya yale aliyoyatenda kwenye utawala wake, anaomba
Watanzania wamsamehe, anaandika Wolfram Mwalongo.
Kinachomfanya kujuta ni hatua ya utawala wake kukabidhi ‘injini ya
uchumi’ wa taifa hili kwa wawekezaji chini ya ‘sera ya ubinafsishaji.’ Mkapa
alikabidhi mashirika ya umma mikononi mwa wawekezaji bila kuwa na mkakati wa
kusimamia ili sera yake iwe na tija kwa taifa.
Rais Mkapa
alihudumia nchi hii kama rais kuanzia mwaka 1995 hadi 2005. Alipokea madaraka
hayo kutoka kwa Rais Ali Hassan Mwingi aliyehudumia nchi kuanzia 1985 mpaka
1995, aliyeanza kuhudumia taifa hili kwenye ngazi hiyo ni Mwalimu Julius K. Nyerere
tangu Uhuru 1961.
Akiwa kwenye
Tamasha la Nane la Kigoda cha Mwalimu Nyerere lililofayika kwenye Ukumbi wa
Nkurumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam jana Mkapa amekiri kwamba, hatua ya
kuleta sera ya ubinafsishaji bila kuweka chombo maalum cha kudhibiti kumesababisha
hasara.
Si mara ya
kwanza kiongozi huyo mstaafu kusema maneno hayo hasa anapozungumzia maswala
mazito katika utawala wake.
“Kukosekana
kuundwa mfumo mzuri wa udhibiti kumesababisha kuwepo kwa watu waliotumia fursa
hiyo kwa maendeleo yao binafsi na si kwa Taifa.
“Kwenye uongozi
wangu kitu abacho mpaka sasa ninajuitia ni kuanzisha sera ya ubinafsishaji na
kushindwa kuweka mfumo au chombo cha kuudhibiti,”amesema Mkapa.
Mara kadhaa
wachumi wa kitaifa wamekuwa wakikosoa utawala wa Mkapa kwa kuita wawekezaji na
kuwapa ‘mali’ za taifa katika misingi mibovu ya uangalizi wake na kusababisha
kuteketea kwa mali hizo. Miongoni mwayo ni viwanda, mashirika ya umma pamoja na
Benki.
Mkapa kwenye
tamasha hilo amesema “kuhusu ubinafsishaji huo ndio kitu naweza kukiri
nilikosea na ninachoweza kuwaomba Watanzania msamaha.”
Mashiriki mengi
ya umma pamoja na viwanda vilivyokabidhiwa kwa wawekezaji kutoka nje vilikufa
na wengine kutumia mali hizo za taifa katika kujipatia mikopo na kufanya mambo
mengine nje ya malengo yaliyokusudiwa.
Hata hivyo,
Mkapa amesema “nilifanya kosa lakini hatuwezi kusema ubinafsishaji haufai kwa
sababu ulisaidia kuleta mabadiliko na na kuongeza uzalishaji katika mashirika
yaliyokuwa yameshindwa kuendeshwa na serikali.”
Ametoa mfano
kwamba, “wakati mimi naingia madarakani viwanda vya sukari vya Mtibwa, Kagera,
na Kilombero vilikuwa vikizalisha tani 120,000 hadi 130,000 lakini wakati
naondoka niliacha vinazalisha tani 300,000.
“Mtibwa ilikuwa
imeishakufa kabisa, lakini tuliweza kukirudisha na baada ya mimi kuondoka
vimeendelea kuzalisha lakini inashangaza kuona miaka 17 wameshindwa kuongeza
uzalishaji.”
Hata hivyo Mpaka
alirudisha lawama kwa Watanzania kwamba, wana hulka ya kuzungumzia zaidi watu
kuliko kuzungumzia sera na kuziboresha ili ziwe na tija kwa taifa.
Kwenye hotaba
yake Mpaka amesema kuwa, Mwalimu Nyerere alishughulishwa katika kutafuta
maendeleo ya Watanzania na kwamba, hakupinga ubinafsishaji kwenye taifa hili.
“Mwalimu Nyerere
alikubali dhana ya ujasiriamali, uwekezaji, ushindani, ubunifu, ufanisi na
utengenezaji wa faida vitu ambavyo viko sambamba na Ubepari,” amesema Mkapa na
kuongeza;
“Vitu alikuwa
anavitaka Mwalimu ni baadhi ya mambo mabaya ya Ubepari ikiwemo unyonyaji na
mgawanyo wa faida usio sawa na ndio maana akaweka Azimio la Arusha akilenga
kuwa na jamii ya usawa isiyo na unyonyaji.”
Akizungumzia
ubinafsishaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) amesema, Mwalimu Nyerere
aliona faida za ubinafsishaji na kwamba, aliona umuhimu wa kuibinafsisha benki
hiyo.
“Kuhusu NBC
Mwalimu si kwamba alikuwa anapinga kuibinafsisha bali ni namna ambavyo inaweza
kuwanufaisha wananchi baada ya kuibinafsisha,” amesema Mkapa.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni