MEYA WA UKAWA KINONDONI AWA MBOGO,AWASHUKIA WATENDAJI WANAOBALISHA HATI ZA VIWANJA,SOMA HAPO KUJUA

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Boniface Jacob akiwaonesha waandishi
wa habari ramani inayoonyesha eneo la makaburi lililovamiwa na taasisi ya
Mkapa Foundation ambalo limegaiwa na manispaa kinyume na taratibu.
Kwa maelezo
ya nyaraka za manispaa zinavyoonyesha, eneo hilo limetolewa wakati baraza
la madiwani likiwa limemaliza muda wake. Cha kushangaza eneo hilo, manispaa
haijaambulia hata shilingi. Na mwisho kabisa mstahiki meya, ameaagiza
kusimamishwa shughuli zozote katika eneo hilo.
MEYA wa
Manispaa ya Kinondoni,Boniface Jacob amewataka watendaji wa manispaa hiyo
kuacha tabia ya kubadilisha hati za viwanja vilivyotengwa kwa ajili maziko na kwenda kwa ajili ya matumizi ya ujenzi wa majengo ya kawaida.Anaandika KAROLI
VINSENT endelea nayo.
Jacob ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam,wakati
alipokuwa akifanya ziara ya kushtukiza kwenye eneo la Kawe jijini hapa ambao
katika eneo hilo kuliibuka mgogoro mkubwa kati Wananchi wa eneo hilo –
Na viongozi
wa watendaji wa Kawe ambapo mgogoro huo ulitokana na eneo hilo kuwepo na
kiwanja kilichokuwa kunatumiwa na wananchi hao kufanyiwa maziko ila kwa sasa
kinadaiwa kuchukuliwa na Taasisi ya
Benjamini Mkapa Foudation kwa ajili ya kuendeleza huduma ya makazi ya Binadamu
jambo lilowachukiza wananchi hao hadi kuifanya ofisi ya Meya kuingilia kati .
Jacob aliwataka watendaji wa manispaa hiyo kuacha tabia ya kubalisha mtumizi ya viwanja vyote
ndani ya Kinondoni vilivyotengwa kwa ajili ya wananchi kufanyia maziko
na kwenda kwenye ujenzi wa Makazi.
Amesema licha ya Manispaa hiyo kugubikwa na kashfa
ya uuzwaji wa viwanja vya wazi vilivyotengwa kwa ajili ya michezo ila
amesikitika na hali ya uuzwaji wa maeneo yalitoengwa kwa ajili ya Maziko jambo
analodai linaichafua manispaa hiyo.

Meya huyo ambaye ni Diwani wa Kata ya Ubungo kupitia
Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema amesema kwa sasa hatakubali chini ya uongozi wake
kuona wakazi wa kinondoni wananyanyashwa kwa kuanyang’anywa viwanja vyao pamoja
na maeneo ya wazi kwa kusema atahakikisha maeneo yote yalioyotengwa kwa ajili
ya huduma yanaendelezwa kwa huduma hizo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni