JESHI LA POLISI LAINGILIA KATI MAPAMBANO YA CHADEMA,ACT-WAZALENDO NA CCM,SOMA HAPO KUJUA
JESHI la Polisi nchini
limeingilia kati ‘vita’ ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Chama
Cha Mapinduzi (CCM), anaandika Faki Sosi.
Taarifa ya Nsato Mssanzya, Kamishna wa Polisi
Operesheni na Mafunzo, Makao Makuu jijini Dar es Slaam imevunja mpango huo wa
jino kwa jino kati ya CCM na Chadema uliotarajiwa kuanza leo.
CCM ilipanga kuingiza
mguu sehemu ambayo Chadema itakuwa imeondoka. Ni baada ya kutangaza ziara ya
kuzidua wananchi kuhusu haki ya kudai nchi kuendeshwa kwa mujibu wa Katiba.
“Jeshi la Polisi
kupitia vyanzo vyake mbalimbali vya habari limebaini kuwa, mikutano hiyo ina
lengo la kuwahamasisha wananchi kutotii sheria za nchi (Civil disorder),”
imeeleza taarifa ya CP Mssanzya kwa vyombo vya habari.
Amekiri kwamba, jeshi
hilo limepokea taarifa kutoka kwa baadhi ya vyama vya siasa wakitaka kufanya
mikutano na maandamano.
“Kwa hali hiyo, Jeshi
la Polisi nchini linapiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara kuanzia
tarehe 07/06/2016 hadi hapo hali ya usalama itakapotengemaa.
“Jeshi la Polisi
linawataka wanasiasa kuacha mara moja kuwashinikiza wananchi kutotii sheria za
nchi. Jeshi la Polisi halitasita kumchukulia hatua kali za kisheria mtu
yeyote au chama chochote cha siasa kitakachokaidi agizo hili,” imeeleza taarifa
hiyo.
Hivi karibuni Chadema
kupitia kwa Benson Kigaila, Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Mafunzo na
Usimamizi wa Kanda alitangaza kuanza kwa ziara ya chama hicho.
Akizungumza na
waandishi wa habari Kigaila alisema, lengo la ziara hiyo
ni kukumbusha wananchi kwamba, nchi inapaswa kuendeshwa kwa mujibu wa
Katiba ya Jamhuri.
Alidai Rais John
Magufuli anaendesha nchi kinyume na taratibu pia Katiba ya Nchi na kwamba,
ziara hiyo imepangwa ili kuzindua wananchi wajibu wa kudai viongozi waongoze
kwa mujibu wa Katiba ya Nchi.
Ziara hiyo ilipangwa
kuanza kutekelezwa tarehe 7 Juni mwaka huu nakuanzia mkoani Shinyanga, Wilaya
ya Kahama.
Na baada ya hapo
kutakuwa na timu mbili zitakazozunguka katika mikoa yote nchini ikiwemo ya
Chato, Bukoba, Geita, Sengerema, Muleba, Meatu, Bunda, Bariadi na kumalizika
Mwanza ambapo timu hizo mbili zitakutana.
“Tangu kuingia
madarakani Rais Magufuli kumekuwa na ukiukwaji wa sheria na katiba, serikali imekuwa
ya mtu mmoja na maamuzi ya mtu mmoja kana kwamba, hakuna wizara husika kitu
ambacho kinawakandamiza wananchi na kushindwa kupata haki zao,” amesema na
kuongeza;
“Hatuta choka kupiga
kelele anapoenda kinyume na kupuuza Katiba ya nchi na tunataka wananchi wa
mtambue na wajue namna ya kudai haki zao. Tangu kuingia kwake madarakani hakuna
maendeleo zaidi ya kulipiza visasi kwa watu ambao hawakumuunga mkono wakati wa
kampeni.
“Rais Magufuli
amevunja na kuvuruga vitu vingi vilivyopo kwenye Katiba ikiwepo sikukuu,
kupanga matumizi ya fedha wakati wizara husika zipo, uvurugaji wa bunge na
mengine mengi yasiyomuhusu,” alisema Kigaila.
Baada ya kauli hiyo,
Christopher Ole Sendeka, Msemaji wa CCM alisema kuwa, chama chake hakitokalia
kimya chochote kitakachoonekana kuipaka matope CCM pia Rais Magufuli
anayetokana na chama hicho.
Ole Sendeka
alinukuliwa akisema kuwa, Chadema kinataka kufanya ziara hiyo kwa ajili ya
kuishitaki Serikali ya Rais Magufuli kwamba ni ya kifashisti na kidikteta.
“Kuanzia Mei 6 mwaka
huu baada ya Kikao cha Kamati Kuu ya Chadema habari zilianza kuandikwa na
gazeti moja la kila wiki kuhusu mikakati ya chama hicho.
“Pia ziliandikwa
makala zikieleza yale yaliyojiri kwenye kikao cha kamati kuu kwamba watakwenda
kuishitaki Serikali Rais Magufuli kuipeleka nchi kifashisti na
inaongozwa kidikteta…,
“Mambo haya yamekuwa
yakirudiwa mara kwa mara si vema kuyanyamazia,” alinukuliwa Ole Sendeka akidai
kwamba, kwake tatizo zi mikutano isipokuwa maudhui yake.
“Kama wataenda
kuyasema mambo kama haya wakitoa mguu nami naweka mguu wangu kueleza wananchi
jinsi Chadema inavyotetea mafisadi,” amesema Ole Sendeka.
Katika taarifa ya
Jeshi la Polisi imeeleza kuwa, chama chochote hakiruhusiwi kufanya mikutano
mpaka pale taarifa mpya itakapotolewa.
·
·
25
·
1
·
·
·
Hakuna maoni
Chapisha Maoni