BAJETI YA MAGUFULI YAWAKERA WABUNGE,SOMA HAPO KUJUA
BAJETI ya serikali kwa Mwaka wa Fedha 2016/17
iliyosomwa jana, imekera wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), anaandika Faki Sosi.
Wabunge hao wameonesha kukerwa
na bajeti hiyo pale Dk. Philip Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango alipogusa
maslahi yao ya kiinua mgongo.
“Mheshimiwa
spika, natangaza msamaha wa kodi ya mapato kwenye malipo ya kiinua mgongo
kinacholipwa kwa wabunge kila mwisho wa muhula wa miaka mitano ili kujenga
misingi ya usawa na haki katika utoaji wa kodi kwa kila mtu anayestahili kulipa
kodi,” amesema Dk. Mpango katika hotuba yake.
Wabunge
wa CCM ambao
ndio waliokuwa wamebaki bungeni kutokana na wale wa upinzani kutoka nje,
walionekana kutoridhia mpango huo jambo ambalo lilizidisha minong’ono na
kusababisha Dk. Tulia Ackson, Naibu Spika wa Bunge kuingilia kati na
kuwatuliza.
Kabla
ya Dk. Mpango kufikia kipengele cha kuondoa msamaha wa kodi kwenye kiinua
mgongo hicho, wabunge walifanya kazi ya kugonga meza kila ambapo msoma bajeti
alipoweka nukta katika usomaji wake.
Hata
hivyo, Dk. Mpango amesema, lengo la serikali ni kufunga mkanda kwenye bajeti
hiyo ili kuhakikisha inafikia malengo yake ya kupata fedha kukamilisha bajeti
yake ya jumla ya Sh. 29.52 trilioni kwa mwaka huu wa fedha 2016/17.
Bajeti
hii iliyosomwa na Dk. Mpango, ndio ya kwanza katika Serikali ya Awamu ya Tano
chini ya Rais John Magufuli.
Pia,
ndio bajeti ya kwanza tangu kurejea kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992
iliyosomwa bila kuwepo kwa wabunge wa vyama vya upinzani ambao walitoka ikiwa
ni mwendelezo wa kugomea vikao vyote vya Bunge vinavyoendeshwa na Dk.
Tulia kwa madai ya kupendelea CCM.
Dk.
Mpango akisoma bajeti hiyo kuanzia jana saa 10 jioni alisema kuwa, bajeti hiyo
imedhamiria kutekeleza ahadi za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais
Magufuli kama zilivyoainishwa katika Ilani ya CCM wakati wa uchaguzi mkuu mwaka
jana.
Lakini
pia amesema inakwenda sambamba na Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano
pamoja na Dira ya Taifa ya Maendeleo.
Dk.
Mpango amesema kuwa, serikali imekusudia kuleta unafuu wa maisha kwa wananchi
wa chini ikiwa ni pamoja na kudhibiti mianya ya rushwa sambamba na ufujaji wa
fedha za umma nchini.
Katika
bajeti hiyo, kodi mbalimbali zimeongezwa ikiwa ni pamoja na kodi ya usajili wa
magari kutoka Sh. 150,000 na kufikia Sh. 250,000 na bodaboda kutoka Sh. 45,000
hadi Sh. 90,000.
Kodi
ya usajili binafsi wa magari imeongezeka kutoka Sh.5 milioni kwa miaka mitatu
hadi Sh. 10 milioni kwa mwaka, pia kodi ya vileo imeongezwa ambapo bei rasmi
itaanza kutumika Julai mosi mwaka huu.
Pia
serikali imepandisha kodi kwenye uingizaji wa nguo na viatu vya mitumba kutoka
nje ya nchi na kwamba, lengo ni kulinda bidhaa za aina hiyo zinazozalishwa na
viwanda vya ndani ya nchi.
Akizungumzia
udhibiti wa fedha za serikali Dk. Mpango amesema kuwa, kuanzia Julai mosi ni
marufuku kwa wizara, taasisi, wakala wa serikali, mikoa na mamlaka za serikali
za mitaa kufanya biashara na wazabuni na wafanyabiashara wengine ambao
hawatotumia mashine za kulipia kodi kwa njia ya kielekroniki (EFDs).
Na
kwamba, mapato ambayo yatalipwa bila kuwepo kwa stakabadhi za mashine hizo ni
lazima ziambatanishwe na ushahidi kwamba, mfanyabiashara ametangazwa
rasmi na Kamishna wa Mapato kutotumia mashine za EFDs.
Katika
hatua nyingine serikali kupitia Dk. Mpango imetangaza kuwa, tayari imetenga
jumla ya Sh. 2.5 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa Mahakama ya Mafisadi.
Uanzishwaji
wa mahakama hii ulikuwa sehemu ya ahadi ya Rais Magufuli wakati wa kampeni za
uchaguzi mkuu mwaka jana.
Pamoja
na hivyo, serikali imetenga Sh. 72.3 kwa ajili ya shughuli za ndani ya Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) huku jumla ya Sh. 44.7 bilioni
zikitengwa kwa ajili ya shughuli za Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
(CAG).
Bejeti
hiyo ni ongezeko la asilimia 7.04 sawa na asilimia 31 ya bajeti ya mwaka wa
fedha 2015/16 ya Sh. 22.49
Hakuna maoni
Chapisha Maoni