ANNA MGHWIRA WA CHAMA CHA ACT-WAZALENDO ATOA NENO TUHUMA ZA WABUNGE KUTOA RUSHWA YA NGONO KUPATA UBUNGE,SOMA HAPO KUJUA
![]() |
Pichani ni Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo,Anna Mghwira (picha na Maktaba) |
Mwenyekiti
wa chama cha ACT-Wazalendo Anna Elisha Mghwira amekili kuwepo kwa vitendo vya
rushwa na ngono katika mchakato wa kuwapata wabunge wa viti maalamu ndani ya
vyama vyao nchini.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Mghwira
aliyasema hayo mwishoni mwa wiki jijini
dar es salaam katika kongamano la wanawake ,katiba na uchaguzi lililoandaliwa
na mtandao wa wanawake nchini lenye lengo la kujadili fursa ,changamo,pamoja na matazamio
ya nafasi ya ubunge wa viti maalumu nchini.
Bi
Mghwira ambaye alikuwa mgombea Rais pee mwakanamke katika uchaguzi mkuu wa mwaka
jana alisema vitendo hivyo vinasababishwa na wanawake wenyewe kutokujiamini
pindi wanapoomba nafasi za kugombea na kutegemea
msaada kutoka kwa wanaume licha ya wenyewe kuwa na uwezo wa kusimama mwenyewe.
“Hata
tukiondoa viti maalumu rushwa ya ngono itaendelea kuwepo nchini endapo wanawake
tutashindwa kujitambua pamoja na kusimama wenyewe”Amesema Mghirwa.
Kwa
upande wao washiriki katika kongamano hilo wamevitaka vyama kubadili mfumo wa sasa wakuwapata wabunge wa viti
maalumu pamoja na kuitaka jamii kubadili fikra za kila mwanamke aliyefanikiwa
kuwa amewetumia rishwa ya ngono kupata nafasi hiyo.
Aidha
wamesema rushwa ya ngono haitaisha nchini kutokana na wanawake kupenda watu
wenye vitu pamoja na wanawake wengi kutojiamini katika kushughuli zao.
Naye
Mkurugenzi wa Mtandani wa Kijinsia kutoka TGN,Lilian Liundi aliwataka wanawake
kujiamini na kuachana na kasumba na kujuaminisha kuwa kila nafasi ya uongozi ndani ya nchi
inapatikana kwa kutua rushwa ya Ngono.
Be
Liundi amesema kwa sasa Jamii inatakiwa kuondoa dhana potofu kwa wanawake
ambayo inamchukulia mwanamke ni kiumbe dhaifu kwa kudai kuwa mwanamke ni mtu
mwenye maono ambayo yanaweza kuibadilisha jamii.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni