WAZIRI NAPE AULA WACHUYA,WABUNGE WAMGALAGAZA,SOMA HAPO KUJUA
ILE kauli kwamba ‘muosha huoshwa’ imedhihiri bungeni
baada ya wabunge kumkalia kooni Nape Nauye, Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, anaandika Faki Sosi.
Jana wabunge hao wamesema
kwamba, Nape ambaye kabla ya Uchaguzi Mkuu mwaka jana, alikuwa akinadi baadhi
ya Mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Tano kuwa mizigo na kwamba, kuzuia
matangazo ya moja kwa moja ya bunge kutazuia wananchi kumpima kama yeye ni mzigo
ama rumbesa.
Miongoni
mwa waliomng’ang’ania Nape ni Mwita Waitara, Mbunge wa Ukonga, Dar es Salaam
(Chadema) ambapo wakati akichangia Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha 2016/17 amesema,
matangazo hayo yangeonesha wazi kwamba Nape ni mzigo ama rumbesa.
Amesema,
Serekali ya Rais John Magufuli inawasukuma wananchi kuomba stakabadi lakini
haitaki wajue namna gani fedha wanazolipia kodi zinavyotumika.
“Nilipoona
amepewa Wizara ya Habari nikajua ataruhusu mojadala ya wazi ili tumuone yeye
kwamba hatokuwa mzigo lakini yeye amekuwa rumbesa,” amesema Waitara.
Kabla
ya Uchaguzi Mkuu mwaka jana, Nape akiwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM) akiwa na Abdurahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM walitembea
nchi nzima wakinadi baadhi ya mawaziri wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete jambo
ambalo lilisababisha Nape kuitwa Vuvuzela.
Zitto
Kabwe, Mbunge wa Kigoma Mjini amelieleza bunge kwamba, wabunge wote wanaounga
mkono bunge kutooneshwa moja kwa moja na hata kusababisha mtafaruku bungeni
wanahojiwa na Kamati ya Maadili ya Bunge.
Nape
amesema kuwa, wabunge kwa pamoja walisomama na kupinga hatua ya serikali kuzuia
matangazo hayo lakini cha kushangaza wengine wamegeuka.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni